Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mama Salma Kikwete baada ya kuapishwa kuwa
mbunge, bungeni mjini Dodoma jana Aprili 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne, Jakakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo
wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma jana Aprili 4, 2017.
Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa kwa mkewe mama
Salma . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mama Salma akiwasili bungeni tayari kuapishwa. (Picha na Raymond Mushumbusi wa MAELEZO)
Mama Salma akisindikizwa na wabunge wanawake kuelekea mbeleya bunge kula kiapo
Mama Salma akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Rais Mstaafu Kikwete kwa wabunge
Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, (katikati), akiwa na mwanaye wa kiume Ally Kikwete, (kushoto) na
msaidizi wake, bungeni mjini Dodoma jana Aprili 4, 2017
Dkt. Kikwete, akiongozwa na Katibu Myeka wa Spika wa Bunge, Bw. Said Yakubu, (kushoto)
Dkt. Kikwdete na mwanaye Ally, (kulia), wakiongozwa na Katibu Myeka wa Spika, Bw. Said Yakubu kuelekea ukumbini Bungeni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.
Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akisalimia
wabunge mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni wa Spika jana Bungeni Mjini
Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mama Devotha Gabriel.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na
Watu wenye Ulemevu Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu cha Bunge kwa kuomba
Bunge kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za kazi kuendelea kwa
awamu ya pili saa kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269