Breaking News

Your Ad Spot

Sep 22, 2017

TCRA: BLOGGERS WOTE WAJISAJILI TBN


Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jones Kilimbe amefungua warsha ya vyombo vya habari vya mtandaoni (online media) ambapo amesisitiza kuwa kutokana na kasi ya ukuaji wa mitandao ya kijamii ni vyema ikatumika vyema kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jones Kilimbe ameeleza kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu sana inabidi matumizi yake yazingatie utu na staha bila kufanya uchochezi wa aina yeyote.


"Mawasialiano ya mtandao (online) yameendelea kukua mpaka sasa kuna online TV  zaidi ya 50 na blogs zaidi ya 150 huku TV zikiwa 32 tu hivyo ni vyema zikatumika vyema" Alisema


Dkt. Kilimbe ameeleza kuwa ukuaji wa mitandao ya kijamii unaonesha kuwa teknolojia hii imepokelewa vizuri kwani taarifa zinapatikana kwa haraka ukiwa na simu ya mkononi tu, hivyo inabidi mitandao hii itumiwe vizuri kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Dkt. Kilimbe ameshauri inabidi uwepo wa sera na kanuni za kufanikisha mitandao hii inatumiwa vyema na ndiyo maana serikali inaandaa utaratibu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.


"Zamani tulikuwa tunasema the power of the pen lakini sasa nguvu hiyo omehamia kwenye mitandao" alisema Kilimbe

Dkt. Kilimbe amesema hawana budi kushirikiana na watumiaji wa mitandao ya kijamii ili teknolojia hii mpya inatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.


"Mitandao ya kijamii inatumika katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ndiyo maana serikali imeamua kuja na maboresho ambayo yatakuwa bora na salama, pia TCRA itakuwa bega kwa bega" alisema Kilimbe


Pia ametoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na chama cha Tanzania Bloggers Network (TBN) kufanya hivyo kwani ni vyema kuwa na chombo kinachosimamia masuala yanayo wahusu na kuwakutanisha pamoja.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages