Breaking News

Your Ad Spot

Jan 19, 2010

SHATCO YAUA NA KUJERUHI MOROGORO

MTU mmoja  amekufa na 32 kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi la SHATCO na roli kugongana leo katika eneo la Lubungo Mikese Barabara  Morogoro-Dar es Salaam.


Makama wa Polisi Thoboas Andengenye, ajali imetokea leo saa 11.45 alfajiri na kwamba aliyekuyfa ametambuliwa kuwa ni  Nyabatuli Hazzi  mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda Thobiasi Andengenye basi lililohusika ni namba T 116 AHF Scania ya kampuni ya SHATCO lilokuwa likitoka Kahama likielekea jijini dar-es-salaam na lilikuwa likiendeshwa na Julius Bernard Mwambata(32) mkazi wa Dodoma.

Alisema chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni mwendo kasi kwa dereva wa roli aina ya fuso kuhama upande wake wa kulia na kuhamia kwenye upande wa kushoto wa basi nakuwa jeshi hilo liangalia uwezekano wa kuwasaidia wasio jeruhiwa kuendelea na safari.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages