Breaking News

Your Ad Spot

Jan 19, 2010

KILELE CHA KAMPENI YA FYATUA CHOO USHINDE

MKURUGENZI wa Afya na Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Elias Chinamo akimpatia maelezo Waziri wa wizara hiyo, Profesa David Mwakyusa, kuhusu picha zilizoshinda katika kampeni ya 'Fyatua Choo Ushinde', wakati wa kilele cha kampeni hiyo, jana kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Washindi kutoka mikoa mbalimbali walijishindia zawadi za simu, sabuni, ndoo , mabeseni na kujengewa vyoo vya kisasa.


MSHINDI wa jumla wa kampeni ya 'Fyatua choo ushinde' iliyokuwa ikifanyika nchini kote,Fatma Ally kutoka mkoani Dodoma, akipokea zawadi zake kutoka kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Profesa David Mwakyusa, wakati wa kilele cha kampeni hiyo,jana kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia nia Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda.BAADHI wa wananchi waliohudhuria kilele cha kampeni ya "Fyatua Choo na ushinde"kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, jana, wakisoma vipeperushi vya lengo la kampeni hiyo.

fULL STORy
NA MWANDISHI WETU

TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na hali duni ya usafi wa mazingira hasa katikamaeneo ya ujenzi wa vyoo bora, imelezwa.

Hayo yalisemwajana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika hotuba iliyosomwakwaniaba yake na Waziri Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa katika kilele cha Kampeni ya 'Fyatua Choo na Ushinde',jana kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Pinda alisema, kutokana na hali kuwa hivyo jitihada mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zimefanyika katika kuinua kiwango cha usafi kwa nchi hizo ikiwemo Tanzania.

Alisemamiongoni mwajuhudi hizoni hatua iliyochukuliwa mwaka 2008 kutangazwa mwaka huo kuwa ni wa Kimataifa wa usafi wa mazingira,lengo likiwa kuunganisha juhudi za Kitaifa na za Kimataifa kuhakikisha malengo kusika yanafikiwa sambamba na lengola Milenia.

"Tamko hili linatokana na ukweli kwamba nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zimeonekana kuwa nyuma katika kufikia malengo hayao na hivyo kuhitaji juhudi za makusudi ilikukabiliana na changamoto hii", alisema Pinda katika hotuba hiyo.

Alisema kulingana na utafiti uliofanywa na Tanzania Household Budget uliofanywa mwana 2005, hali ya matumizi ya vyoo mijini ni asilimia 98 huku vijijini ikiwa asilimia 86 na vyoo vingi havina viwango vya ubora unaoridhisha.

Pinda alisema, itafiti uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umebaini kuwa asilimia 47.2 tu ndio vyoo bora. Katika takwimu hizo asilimia 42.8 ya vyoo vulivyopo ni duni na asilimia 10 ya kaya hazina vyoo kabisa.

" Kutokana na takwimu hizo inabidi tujiulize sisi wenyewe kuwa hawa watu ambao hawana vyoo wanajisaidia wapi,ni dhahiri hawa ndio watakuwa wanajisaidia vichakani na katika sehemu zisizokubalika", alisema Pinda.

Alisema, mikoa minane nchini ilipata matukio ya milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu am,bapo hadi kufikia Januari 4, mwaka huu kulikuwa na wagonjwa 6,972 na vifo 126,mikoa ya Dar es Salaam, na Tanga ikiongoza kuwa na wagonjwa wengi.

Katika kilele hicho, Profesa Mwakyusa alikagua picha zilizoshinda katika shindano la kampeni hiyo, na baadaye kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi kutoka mikoa kadhaa.

CIAO

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages