.

SERIKALI KUWASILISHA TENA KIKAO CHA CITIES MAOMBI YA KUUZA MENO YA TEMBO ILIYONAYO KATIKA MAGHALA

Apr 1, 2010

SERIKALI  itawasilisha tena maombi yake ya kuuza meno ya tembo yaliyoko kwenye maghala ya serikali licha ya mkutano wa wanachama wa mkataba wa kudhibiti biashara ya kimataifa ya wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES) kuikatalia.
    Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga amesema leo mjini Dar es Salaam,  kuwa katika mkutano wa 15 wa CITES uliofanyika Doha, Qatar, ilidaiwa kuwepo kwa kasoro kadhaa na hivyo Tanzania kukosa theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kuweka kupata kibali.
    “Tanzania itafanya marekebisho muhimu ya kasoro zilizobainishwa ili iweze kuwasilisha tena maombi yake ya kuuza meno ya tembo,” alisema Shamsa na kubainisha baadhi ya mambo yatakayofanyiwa kazi ni kuongeza mikakati ya kudhibiti ujangili wa tembo nchini na kuzidisha juhudi za kuzuia meno ya tembo kuingia au kutoka nje ya mipaka ya nchi.
    Shamsa alikuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kwa nini Tanzania haikukukubaliwa kuuza meno ya tembo ambayo ni tani 89.8 sambamba na Zambia ambayo nayo iliomba kuuza tani 21.7.
   Alisema wapinzani waliokataa meno hayo yasiuzwe walidai kuwa taarifa za vyombo mbalimbali vya uhifadhi na utekelezaji wa mkataba wa CITES, meno mengi ya tembo ambayo yanakamatwa na vyombo vya doka katika nchi balimbali husisani bara la Asia, yaneonekana kutokea Tanzania.
   Kwa tathmini hiyo, udhibiti wa usafirishaji haramu wa meno ya tembo ndani ya Tanzania umeonekana haujafikia kiwango kinachokubalika.
   Shamsa alisema kuwa nchi hizo pia zilihofia kuwa iwapo Tanzania na Zambia zitaruhusiwa kuuza meno ya tembo, kasi ya ujangili itaongezeka kwa madai kwamba wafanyabiashara haramu wataendelea na itakuwa kama kufunua upya mlango wa biashara hiyo.
   Alisema serikali inahitaji kuuza meno hayo ili pesa zitakazopatakana karibu dola za marekani milioni 20 zitumike kwa uhifadhi na maendeleo ya taifa.
   Waziri alisema kuwa hatua ya serikali kuuza meno hayo ilikuja baada ya kuona ina vigezo vyote vinavyokubalika kwani idadi ya tembo nchini imeongezeka kutoka 55,000 mwaka 1989 hadi kufikia 110,000 mwaka jana.
   Kwa mujibu wa sheria za CITES wanyama na mimie vimegawanywa katika makundi matatu kulingana na kiwango au hadhi ya uhifadhi kwa kuzingatia ngazi hatari ya kutoweka duniani.
   Katika kundi la kwanza, ambao kwa mtazamo wa dunia wako kwenye hatari kutoweka au wanaweza kuathiriwa na biadhara wakatoweka ni tembo, Faru, Duma na Chura wa Kihansi. Viumbe hawa hawaruhusiwi kufanyiwa biashara yoyote ya kimataifa.
   Alisema serikali itaendelea kuhifadhi men ohayo, licha ya kwamba maghara ni madogo na kwamba haitakubali kuyachoma kama ilivyowahi kufanya nchi za Kenya na Zambia katika miaka iliyopita ambapo walipewa pesa kidogo.
    “Meno yetu yana thamani kubwa na yatasaidia sana katika masuala mbalimbali, hivyo kuyachoma moto haiwezekani, kwani hata tukifanya hivyo hayawezi kugeuka tembo,” alisema.


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dhamsa Mwangunga akizungumza na Waandishi wa habari, leo Dar es Salaam kuhusu yaliyojiri katika mkutano wa 15 wa CITES uliofanyika mjini Doha, Qatar hivi karibuni. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ladislaus Komba.OFISA Wanyamapori Mkuu wa kitengo cha Uzuiaji ujangili, John Muya akionyesha meno ya tembo yaliyohifadhiwa katika ghala la serikali kwenye ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam, leo. Meno ya tembo katika ghala hilo
 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª