.

CCM Iringa yaanza kuzibana Halmashauri juu ya utekelezaji wa Ilani

Apr 1, 2011

NA FRANCIS GODWIN,  IRINGA
Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa  Iringa  kimeanza  kufuatilia  utekelezaji  wa Ilani ya uchaguzi  katika Halmashauri ya Manispa ya Iringa kwa kutembelea miradi mbali mbali ya kimaendeleo.

Katibu  wa  CCM ,mkoa wa Iringa Mary Tesha amesema kuwa lengo la ziara  hiyo ni kuona jinsi ambavyo ilani ya CCM ilivyoanzwa  kutekelezwa mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana .

Amesemea kuwa katika ziara  hiyo CCM imefurahishwa na utekelezaji wa Ilani yake katika Manispaa ya Iringa na kutaja baadhi ya maeneo ambayo yamefanywa  vizuri kuwa ni pamoja na miradi ya ujenzi  wa sjhule za  sekondari,vituo vya afya na miradi mingine ya kimaendeleo.

Katika ziara  hiyo iliyoanza Manispaa ya Iringa CCM mkoa pamoja na kamati ya utekelezaji ya wilaya ya Iringa mjini ikiongozwa na katibu wake Charley Charlesy  kwa upande wa Manispaa ya Iringa  imetembelea  shule ya  sekondari ya mazoezi Kleruu, kituo cha afya Ngome , shule ya  sekondari Kihesa  ,Mtwivila na kufanya mkutano na wananchi wa  kijiji cha Nduli.


Pamoja na  kupongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na uongozi wa shule  hiyo na wananchi wa kata ya Gangilonga katika  kuendeleza  shule  hiyo bado katibu   wa  CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha aliutaka uongozi  wa  shule ya  sekondari Mazoezi Kleruu  kueleza sababu ya  shule yake kukosa  walimu .

Alisema  kuwa kimsingi shule  hiyo ni sehemu ya nyenzo za kufundishia walimu katika  chuo cha ualimu Kleruu  na ndio  sababu ya  serikali  kujenga  shule  hiyo ndani ya majengo ya chuo cha ualimu Kleruu  hivyo uongozi wa  shule  hiyo kulia juu ya tatizo la walimu ni jambo la kushangaza .

“Tumefurahishwa  sana na jitihada mbali mbali  zinazofanywa na kamati ya ujenzi na wananchi wa kata hii ya Gangilonga pamoja na Manispaa ya Iringa katika  kuboresha elimu Manispaa ya Iringa …ila kwa  hili la kukosa   walimu wa  kutosha hapa shule ya  sekondari Kleruu tunaomba maelezo ya  kutosha” alisema katibu  huyo.

Kwani alisema kuwa  lengo la ziara  ya CCM katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni  kutaka kuona jinsi ambavyo ilani ya CCM ilivyoanzwa  kutekelezwa baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010 ili kuona changamoto mbali mbali zinazokwamisha utekelezaji wa Ilani hiyo na mafanikio ya utekelezaji wa  kipindi kifupi ambacho Rais Jakaya  Kikwete ameingia madarakani.

Kwa upande  wake mstahiki Meya  wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alisema  kuwa Halmashauri  hiyo ina jukumu  kubwa ya  kusimamia  kwa umakini utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwa siku ya kwanza kabisa ya kuanza kwa baraza  jipaya la madiwani mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo alikabidhiwa Ilani ya CCM kama  kitendea kazi namba moja katika kutekeleza ahadi za  serikali iliyopo madarakani.


Kwa upande  wake mkuu wa  shule  ya Mazoezi Kleruu Yoram Mponzi alisema  kuwa  shule  hiyo ina jumla ya walimu 17 japo awali  kabla ya  walimu 12 kwenda masomoni ilikuwa na walimu  28.

Hata  hivyo alisema kuwa sababu  kubwa iliyopelekea shule  hiyo  kuwa na upungufu  wa  walimu ni kutokana na utaratibu mpya wa  wizara ya elimu ambapo ulisitisha  utaratibu wa  shule  hiyo kuchagua  walimu wanaohitimu katika  chuo  hicho kufundisha shule hiyo kabla ya  kupangiwa  walimu na katibu mkuu wa wizara ya elimu.

Hata hivyo alisema kuwa sababu kubwa iliyopelekea shule hiyo kuwa na upungufu wa walimu ni kutokana na utaratibu mpya wa wizara ya elimu ambapo ulisitisha utaratibu wa shule hiyo kuchagua walimu wanaohitimu katika chuo hicho kufundisha shule hiyo kabla ya kupangiwa walimu na katibu mkuu wa wizara ya elimu.
Pia alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002 ina jumla ya wanafunzi 842 wakiwemo wasichana 412 na wavulana 430 na ina kidato cha 1-IV.

Vyumba vya madarasa vilivyopo ni 16 maktaba ipo japo haijakamilika ,maabara vyumba 2 havijakamilika na chumba kimoja kiko kwenye hatua ya umaliziaji ,matundu ya vyoo vya wanafunzi 16.
Huku matundu ya walimu ya shule hayopo kabisa zaidi ya kutumia yale ya chuo cha ualimu pekee.

Katika hatua nyingine wafanyakazi wa  zahanati ya Ngome wamelalamikiwa kwa kutoa majibu mabaya  kwa wagonjwa pindi wafikapo kupata huduma za afya
Malalamiko hayo yametolewa mbele ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa Mary Tesha wakati alipofanya ziara yake katka zahanati hiyo ikiwa ni mikakati ya kutimiza ilani ya chama hicho

Mwenyekiti wa matta wa Ngome Mario Mponzi amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya wauguzi wa zahanati hiyo kutoa majibu yasiyofaa kwa wagonjwa hali inayopelekea wananchi katika eneo hlio kukikimbilia katika hospitali ya mkoa kufuata huduma wanazo hitaji

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª