.

ADAMU LUSEKELO HATUNAYE DUNIANI TENA

Apr 1, 2011

TASNIA ya habari imepata pigo la aina yake kutokana na mwandishi mahiri wa siku nyingi  Adam Lusekelo (54) kufariki dunia usiku wa kuamkia leo, wakati akipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili mjini Dar es Sakaam.

Scolastica Lusekelo ambaye ni mjane wa marehemu, amesema leo kwamba afya ya marehemu ilidhoofu usiku wa jana ndipo akaamua kumpeleka hospitali ya Aga Khan ambao walimpa uhamisho kwenda Muhimbili  kutokana na kuzidiwa.

Kaka wa marehemu, Ben Mwakang’ata alisema mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Ubungo na kuwa kuna uwezekano mwili wa marehemu ukasafirishwa kesho kuelekea Rungwe, Mbeya.
Marehemu Lusekelo ameacha mke na watoto watatu, wawili wa kike na wa kiume.

Katika uhai wake Lusekelo, alifanya kazi kwa muda mfupi na TSN katika miaka ya 1980 kabla ya kujiunga na BBC kama mwandishi wa habari akiandikia Dar es Salaam.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª