.

LEO NI LEO SIMBA NA TP-MAZEMBE UWANJA WA TAIFA

Apr 3, 2011


Kikosi cha Simba
 Timu ya Simba inashuka dimbani leo kumenyana na timu machachari ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, TP Mazembe, katika mechi ngumu na muhimu ya Ligi ya mabingwa Afrika.
     Mechi hiyo inakitwa kuanzia saa 9.30 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba inatakiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi hiyo, kwa kuwa katika mechi ya kwanza zilipokutana timu hizo nchini DRC, ilichapwa mabao 3-1.
Kikosi cha TP Mazembe


 Klabu ya Simba, chini ya Kocha wake, Mzambia Patrick Phiri inawatara wachezaji wake mahiri wakiwemo  Mussa Hassan Mgosi, Emmanuel Okwi, Mbwana Samata na Rashid Gumbo. kufanya kweli ili kuibuka na ushindi.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª