.

SIMBA NA TP MAZEMBE ZAKAMIANA

Apr 2, 2011


 Kocha wa Simba, Patrick Phiri (kulia) na Meneja wa Timu ya TP-Mazembe, Tzediriki Kitenge (kulia), kila mmoja akionyesha kuwa na mawazo kivyake, kuhusu mechi ya timu zao, itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Phiti na mwenzake walikutana kwenye ukumbi wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kueleza kila mmoja alivyoandaa timu yake, ili kuweza kuibuka na ushindi katika mechi hiyo ambayo ni ya marudiao. Katika mechi hiyo Simba inahitaji ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa katika mechi ya awali Simba ilifungwa mabao 3-1. (Picha kutoka Blogu ya Dina Ismail).

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª