.

AJTC BINGWA WA BONANZA LA TISA LA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI

Jun 30, 2014

mwenyekiti wa Taswa Taifa Juma  Pinto akiwa akiwa anakagua timu ya mpira wa pete kutoka AJTC kabla ya mechi ya fainaili kuchezwa

washabiki wa timu ya AJTC wakiwa wanashangilia mara baada yakukabidhiwa kombe katika bonanza la Taswa


Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway akitoa  neno ndani ya bonanza hilo

Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL akiongozana na meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Mega Trade Investment Godluck Kway kukagua timu ya netball ya chuo cha uandishi wa habari AJTC 

IMG-20140629-WA0000kikosi cha timu ya mpira wa miguu kutoka cho cha AJTC

IMG-20140629-WA0002

IMG-20140629-WA0003Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa AJTC Bw. Alli Ahmedi akikabidhiwa kombe la ubingwa na Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL

IMG-20140629-WA0004


 

Timu za Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, lililofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Katika bonanza hilo, ambalo mgeni rasmi alikuwa, Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma Pinto  jumla ya timu  10 zilishiriki na  liliandaliwa na Taswa Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique.

Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha  uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5.

Mgeni rasmi Pinto ambaye pia ni Mjumbe wa bodi vya Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa  soka alipewa kikombe, pamoja na fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.

Mshindi wa pili wa soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa kikombe na fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.

Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (TBL), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel,

Timu zilizoshiriki ni Radio 5, timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara, Salam Club, IMS na  Taswa Arusha  ambayo iliibuka na ushindi katika kukamata kuku.

Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi  nzuri waliofanya.

“Nachukuwa fursa hii kuwapongeza sana Taswa Arusha kwa kuandaa bonanza hili kwani halifanyiki sehemu nyingine nchini”alisema

Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi TBL kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.

Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kuendelea kulidhamini.

WAZIRI WA MALISILI NA UTALII AZINDUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO (SITE)

2a
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Bw. Goefrey Tengenea wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na maofiza wenzake wa TTB wakati wa hafla hiyo.
................................................................................................
(HOTUBA YA MH. WAZIRI RAZALO NYALANDU WAKATI WA UZINDUZI WA SITE)
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati, kwa wageni wote mliofika katika tukio hili muhimu ambapo nitatambulisha kwenu kuanzishwa kwa onesho jipya la utalii la kimataifa litakalojulikana kwa jina la Swahili International Tourism Expo (S!TE).
1. Sekta ya Utalii ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hasa kwa kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi kama vile usafirishaji, viwanda na biashara, kilimo, sanaa za mikono na kadhalika. Sekta ya utalii ina uwezo wa kuongeza ajira kwa haraka zaidi na inatambulika kwamba kila mtalii mmoja anapokuwa nchini huchangia takribani nafasi 12 za ajira za aina mbalimbali. Aidha, Utalii ni tasnia muhimu katika kuongeza kipato na kupunguza umasikini, kukuza mahusiano ya kijamii na vile vile katika kutunza na kuendeleza maeneo ya kihistoria na maliasili. Hapa nchini, katika kipindi cha kati ya mwaka 2002 na 2013, utalii wa kimataifa umekuwa kwa zaidi ya asilimia 50%, kutoka watalii 575,000 mwaka 2002 wambao waliliingizia taifa Dola za Marekani milioni 730 hadi kufikia watalii 1,135,884 mwaka 2013 ambao waliingizia taifa Dola za marekani Bilioni 1.81.
2. Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vya maliasili na utamaduni vya kipekee. Kutokana na kuwepo kwa vivutio hivi, taasisi ya Kimataifa ya World Economic Forum katika taarifa yake ya ushindani kwenye tasnia ya Utalii (Travel and Tourism) imeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) duniani ikiongozwa na Brazili kwa kuwa na mazingira asilia yenye Urithi asilia wa kimataifa, wingi wa wanyamapori na ardhi kubwa iliyo hifadhiwa. Hakika, ni ukweli usiopingika kwamba katika vivutio saba vya maajabu ya asili katika bara la Afrika, vitatu vinatoka Tanzania. Huu ni ushuhuda kwamba juhudi zetu za kuhifadhi mazingira zinazaa matunda. Hivi sasa Bonde la Ngorongoro; hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na Mlima Kilimanjaro ni vivutio ambavyo vimeorodheshwa katika Maajabu saba ya asilia barani Africa.
3. Hata hivyo, hatuwezi kutegemea tu uwingi na ubora wa vivutio hivi vya utalii peke yake. Ni muhimu kuongeza juhudi zaidi kuliko wakati mwingine wowote, ili kujenga uelewa wa utajiri huu kidunia. Kama taifa, tunahitaji juhudi na mikakati zaidi ili kutangaza vivutio vyetu.
4. Kwa kuzingatia umuhimu wa kuendelea kutangaza utalii wetu na kuifaya Tanzania iweze kushindana kimataifa, mnamo mwezi Februari, 2013, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), iliingia makubaliano na kampuni inayojulikana kama Pure Grit Project and Exhibition Management LTD, hapo mwanzo ilijukana kama Witch & Wizard Creative (Pty Ltd) ili kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa nchini Tanzania yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo -S!TE), ambayo yataanza rasmi Mwezi Oktoba, 2014. Pure Grit Project and Exhibition Management LTD ni kampuni inayoendesha maonesho ya utalii ya INDABA ambayo ni maonesho ya tatu kwa ukubwa duniani. Onesho la S!TE litafanyika hapa Dar es salaam, mwezi Oktoba kila mwaka katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na kujikita zaidi katika kuvutia washiriki kutoka ndani nan je ya nchi.
5. Mkoa wa Dar es Salaam umechaguliwa mahsusi kuwa eneo la kufanyika kwa onesho la S!TE kutokana na sehemu ulipo Mkoa huo kijiografia, na uwepo wa miundombinu bora na huduma nzuri zinazofaa kwa kuendesha au kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa.
6. Hadi kufikia Juni 2014, hali ya maandalizi ya onesho hili ni kama ifuatavyo.
6.1 Mwenendo wa idadi ya washiriki hadi sasa: Zaidi ya asilimia 50% ya nafasi za maonesho hayo tayari zimejazwa kwa kuchuliwa na makampuni binafsi na Bodi za Utalii za nchi mbalimbali. Aidha, kuna idadi kubwa na ya kuridhisha ya maombi ya washiriki inayoendelea kuandaliwa. Lengo ni kwamba ifikapo katikati ya mwezi Agosti, 2014 tuwe tumetumefikia asilimia 100.
6.2 Programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii: Katika kuhakikisha kuwa onesho hili linakuwa ni fursa ya kuwaunganisha wafanyibiashara ya Utalii wa Tanzania na masoko ya Utalii, S!TE itakuwa na programu maalum (Hosted buyer and travel writer programme) ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii na waandishi wa habari za utalii (Tour Operators, Wholesalers, Packagers and Travel Agents and Travel Writers) na kuwapangia ratiba maalum ya kuonana na washiriki wa maonesho hayo ili kuwawezesha kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Mawakala hao wapatao ishirini na wandishi wa habari kumi watagharimiwa (hosted) na S!TE.Hadi kufikia Juni 2014,mawakala 13 kutoka Marekani, Australia, Ujerumani, Uholanzi, India, Mexico, Norway na China wamethibitisha ushiriki wao.
6.3 Utangazaji wa Onesho la S!TE: Onesho la S!TE lina tovuti ijulikanayo kama www.site.co.tz. Tovuti hii imeandaliwa ili kukidhi maudhui ya onesho lenyewe ambapo inataarifa nyingi zinazoweza kumfanya yeyote anayetembelea tovuti hiyo kupata taarifa zote muhimu kwa muda mfupi. Kwa mfano tovuti inatoa taarifa za ukumbi wa onesho, mabanda ya maonesho yatayojengwa na kumruhusu mteja kuchagua eneo kulingana na uwezo wake. Aidha, tovuti hii ambayo pia imeunganishwa na ukurasa wake wa Facebook, inapatikana kwa lugha mbalimbali
7. Pamoja na kuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha utalii katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, S!TE ina lengo la kuunganisha wafanya biashara wa Utalii wadogo na wa kati wa Tanzania (Small and Medium Tourism Enterprises - SME’s), na masoko ya utalii ya kimataifa. Ni ukweli kwamba SME’s za kitanzania zina uwezo mdogo wa kimtaji wa kuweza kufikia masoko ya utalii ya kimataifa. Kupitia S!TE, hasa kupitia programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii, itasaidia katika kutatua changamoto hii.
Naomba watanzania kuchangamkia fursa hii muhimu katika kukuza biashra ya Utalii nchini.

BRAVO JOB CENTRE YAPELEKA VIJANA KUMI KUFANYA KAZI DUBAI, WATANO NI WA TRIP YA KWANZA YA MADEREVA

 Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo Job Centre Agency, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akimpatia  mkazi wa Zanzibar, Badrudin Alidina tiketi ya ndege  na vibali vya kwenda kufanya kazi ya udereva Dubai, Falme za Kiarabu,  katika hafla iliyofanyika Keko jijini Dar es Salaam ambapo pia wanawake watano walipatiwa tiketi na vibali vya kwenda kufanya kazi  mbalimbali Qatar Uarabuni.
Dereva,  Maneno Tamba akipokea tiketi na vibali hivyo kutoka kwa Mtemvu
 Hamud Ramadhan akipokea tiketi na vibali vya safari kwenda kufanya kazi ya udereva Dubai
Dereva Salum Rashid akikabidhiwa tiketi na vibali kwa ajili ya safari hiyo
 Dereva, Khatib Mohamed Waziri akikabidhiwa na Mtemvu  tiketi na vibali  kufanya kazi ya udereva Dubai.
 Mkazi wa Dar es Salaam, Rahma Salehe akipokea tiketi na vibali vya kwenda kufanya kazi Qatar, Falme za kiarabu
Mkazi wa Dar es Salaam, Hindu Khamis akipokea tiketi na vibali vya kwenda kufanya kazi Qatar, Falme za kiarabu

Jun 29, 2014


JK AREJEA NCHINI BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA MJINI MALABO EQUTORIAL GUINEA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Malabo Equtorial Guinea ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) uliomalizika jana.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange Picha na Freddy Mar

RAIS ALHAJ DK. ALI MOHAMMED SHEIN ATROA SALAM ZA KUANZA MFUNGO MTUKUFU WA RAMADHANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa salamu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa  Wananchi  wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla,pia aliwatakia mfungo mwema  wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya ibada mbali mbali.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.].

TAMWA KUPAMBANA NA ULEVI WA KUPINDUKIA

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leoMkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea. Mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendeleaBaadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani). Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani).Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leoBaadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.

 KITUO cha Usuluhishi (CRC) kinachofanya kazi chini ya Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) kimejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha kinapambana na matumizi ya pombe kupindukia kwa jamii suala ambalo limezidisha vitendo vya ukatili wa jinsia unaofanywa na watumiaji pombe kupindukia.

 Akizungumza na wahariri wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka alisema utafiti uliofanywa na Shirika la IOGT International unaonesha kuwa kiwango cha unywaji pombe jijini Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake huku ikibainika kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya vitendo vya ukatili na matumizi ya pombe kupita kiasi.

 Bi. Soka alisema takwimu zinaonesha kuwa wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha vipigo, kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77, huku kiwango cha ukatili kwa wanawake ambao waume ama wenzi wao hawanywi pombe ni asilimia 33.

 "...Utafiti uliofanywa na shirika la IOGT International unaonyesha kwamba kiwango cha unywaji pombe katika jiji la Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake...lakini takwimu kutokana na utafiti wa Demographia na Afya Tanzania (TDHS) 2010...unaonesha wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha kipigo/kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77," alisema.

 Aidha aliviomba vyombo vya habari kushirikiana na TAMWA kutoa elimu kwa jamii kupunguza matumizi ya pombe kupindukia kwani licha ya ukatili huo familia pia zimekuwa zikiathirika kiuchumi juu ya matumizi ya pombe huku baadhi ya watoto wakikosa huduma za msingi kutoka kwa baadhi ya wazazi ambao ni walevi kupindukia.

 Alisema TAMWA inatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unaosababishwa na pombe huku lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha maisha ya wanawake na watoto yanaboreshwa kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia.

Hata hivyo alisema tayari chama hicho kimeanza kufanya utafiti mwingine katika Wilaya ya Kinondoni kuangalia madhara yanayotokana na unywaji wa pombe kupindukia ili kuangalia hali halisi ya matumizi ya pombe eneo hilo na madhara ambayo yamekuwa yakitokana na matumizi hayo.

Alisema malengo mengine ya mradi ni pamoja na kuboresha maisha ya wanawake na watoto kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe katika wilaya ya Kinondoni na pia kujenga uelewa miongoni mwa jamii juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa pombe kupindukia.

 Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA aliongeza kuwa mapambano hayo pia yatasaidia, kukabiliana na matumizi ya pombe na kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu ukatili dhidi ya wanawake unaotokana na matumizi ya pombe, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa jamii kukabiliana na ukatili unaosababishwa na unywaji wa pombe dhidi ya wanawake na watoto. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

BARAZA LA MITIHANI LAPANGUA MFUMO MZIMA WA KUPANGA MADARAJA YA UFAULU KIDATO CHA NNE NA SITA 2016.

Jun 28, 2014

Matokeo ya Mtihani wa Majaribio (Mock) kwa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu na Kidato cha Sita mwakani, yatachangia alama 10 za Alama Edelevu (CA).

 Kwa utaratibu huu, matokeo ya mwisho ya mtahiniwa, yatatokana na asilimia 30 ya Alama Endelevu na asilimia 70 ni mchango wa Alama za Mtihani wa Taifa.

Asilimia 30 za Alama Endelevu, zitapatikana kutokana na mitihani mbalimbali.

Kwa Kidato cha Nne mwaka huu, alama hizo zitatokana na matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili ambao utakuwa na alama 10, matokeo ya kidato cha tatu muhula wa kwanza na wa pili alama tano, matokeo ya mtihani wa majaribio (mock) wa Kidato cha Nne ni alama 10 na majaribio ya kazi alama tano.


Utaratibu huu umetokana na viwango vipya vya ufaulu, vilivyoainishwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwenye kitabu cha Mwongozo wa Matumizi ya Viwango vya Ufaulu na utaratibu wa kutunuku matokeo ya kidato cha nne na sita.


Kwa Kidato cha Sita, zitatokana na matokeo ya mtihani wa Kidato cha Tano muhula wa kwanza na pili alama 15, matokeo ya 'mock' alama 10 na kazi mradi itakuwa ni alama tano.


“Katika somo ambalo mtahiniwa hakufanyia Kazi za majaribio, alama za matokeo ya Mitihani ya 'Mock' ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita, itachangia alama 15 badala ya 10 zilizoainishwa,” imefafanua sehemu ya mwongozo huo.

Katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana na Kidato cha Sita mwaka huu, mchanganuo wa alama 30 za Alama Endelevu ni alama 15 zinazotokana na matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili, asilimia 10 ilitokana na maendeleo ya mitihani ya kidato cha Tatu muhula wa Kwanza na Pili na matokeo ya muhula wa Kwanza Kidato cha Nne na kazi za majaribio asilimia tano.

Kwa Kidato cha Sita, alama endelevu ni matokeo ya Kidato cha Tano kwa mihula yote miwili ni alama 15, muhula wa kwanza wa Kidato cha Sita ni asilimia 10 na kazi za majaribio ni asilimia tano.

Aidha, Baraza limebadili utaratibu wa kupanga madaraja ya kufaulu, kutoka mfumo wa Pointi na kuwa wa Wastani wa Alama za Mtahiniwa (GPA).

Mfumo unaotumiwa sasa wa pointi, huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa kwa masomo aliyofaulu zaidi, na kupanga madaraja kuanzia la kwanza hadi la nne.

Madaraja ya mfumo wa GPA, hupangwa katika utaratibu wa Distinction, Merit, Pass na Fail. Daraja la Distinction ni la ufaulu wa juu zaidi na daraja Pass ni ufaulu wa chini.

Mtahiniwa hutunukiwa madaraja A, B+, B, C, D, E au F kutegemeana na ufaulu wake katika somo ambapo uzito wa alama katika madaraja A = 5, B+= 4, B = 3, C=2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.

Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo, endapo atapata Daraja D ambayo ni sawa na uzito wa alama moja. Ukokotoaji wa jumla ya GPA ya mtahiniwa hufanyika kwa kuzingatia masomo, ambayo mtahiniwa amefaulu angalau kwa daraja D na kuendelea (D, C, B, B+ na A).

GPA anayopata mtahiniwa hutokana na wastani wa pointi alizopata katika masomo saba aliyofanya vizuri zaidi kwa Mtihani wa Kidato cha Nne au masomo matatu ya mchepuo kwa Mtihani wa Kidato cha Sita.

Aidha, GPA ya mtahiniwa huandikwa katika nafasi moja ya desimali ambapo nafasi ya pili ya desimali hukadiriwa katika makumi yaliyokaribu.

Mfano, mtahiniwa mwenye GPA ya 3.15 itakuwa sawa na 3.2 na mtahiniwa mwenye GPA ya 3.14 itakuwa sawa na 3.1.

Muundo wa madaraja ya GPA kwa kidato cha nne, Distinction ni 3.6-5.0, Merit 2.6 -3.5, Credit 1.6-2.5, Pass 0.3-1.5, Fail 0.0-0.2 wakati Kidato cha sita ni Distinction 3.7-5.0, Merit 3.0-3.6, Credit 1.7-2.9, Pass 0.7-1.6, Fail 0.0-0.6

MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA VIPI CCM ITAWABWAGA, ASHANGAA KUAMBIWA ANA MASLAHI BINAFSI KUWATETEA MAMALISHE

Jun 27, 2014

NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE
BUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.

Amesema, uhakika huo anao na hata wapinzani wenyewe wanajua hilo, kwa kuwa hawaizidi CCM kwa weledi wa kisiasa, kwa akili wala wingi wa wanachama.

Mtemvu amsema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke, kilichofanyika leo, Juni 27, 2014, kwenye Ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo, mjini Dar es Salaam.

"Wapinzani baada ya kuona kuwa hawatuwezi kwa kila chama kivyake, sasa mnaona wanavyotapatapa, mara eti huo Ukawa walioanzisha wanataka pia kuutumia kwenye chaguzi, kuweka mgombea mmoja mmoja kwa wote, mimi bado naamini hata wafanyeje CCM itawabwaga tu", alisema Mtemvu.

Mtemvu alisema, pale ambapo wapinzani wamekuwa wakipenya na kunyakuwa ubunge au udiwani ni pale ambapo CCM wenyewe wanakuwa wamejichanganya.

"Ikifika acheni mambo ya kuanza mizozano ya ndani kwa ndani kutokana na makundi ambayo husababishwa na baadhi ya wagombea au wanachama wanaowataka wagombea kwa lazima, tukiachana na hili nawahawakikhieni wapinzani hawapati hata kiti kimoja cha cha mtaa", alisema Mtemvu.

Mtemvu aliwataka wana-CCM pia kuachana na mambo ya kushughulika tu na wanaotaka nafasi ambao wana fedha, akisema, kufanya hivyo kunasababisha baadhi kuwa wagombea kutokana na uwezo wa fedha tu na siyo wa uongozi.

Aliwataka mtu anapowajia kwa fedha kuzipokea na kuzila, lakini wakati waanapofikia maamuzi muhimu kwenye uchaguzi wahakikishe wanachagua yule wanayemfahamu kwa thati kwamba anao uwezo wa uongozi.

Alisema, wapo baadhi ya wanachama wa CCM wanao uwezo wa kuongoza lakini hawana fedha, hivyo watu wa aina hiyo wasitoswe kwa sababu ya ufukara wao.

Mtemvu alisema kiongozi mwenye uwezo ni yule anayekubalika na watu, saa zote yupo na watu na anajali maslahi ya wanyonge siyo wale anaowajua kuwa ni wake tu.

"Mfano ni kama hivi tunavyofanya sasa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam. Kila mara tunapigania wanyonge, juzi nimepambana kuwatetea mamalishe wasifukuzwe hovyo, japo baadhi ya watu tena waliopewa malmaka na Rais waknibeza eti nina maslahi binafsi, khaa, yaani mimi niwe na maslahi na mamalishe huu kama siyo uzushi ni nini?" alisema Mtevu.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya Kurasini, wakati wa mkutano huo leo
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo. Habari Picha na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog

FARIDA FOUNDATION YATOA MISAADA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA NA KWA WALEMAVU ENEO LA UBUNGO DARAJANI

 Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi moja ya msaada kwa kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle,Huku wafanyakazi wengine wa Hospitali hiyo wakishuhudia.
 Bi Farida Abdul Akikabidhi bandeji kwa ajili ya kufungia wagonjwa kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle akipoke Ndoo zitakazotumika kwa ajili ya kuhifadhia uchafu katika Hospitali hiyo,ambazo zilitolewa kama Msaada na Farida Foundation
 Bi Farida Abdul akimuonyesha kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle Vifaa ambavyo vimeletwa kama msaada kwenye Hospitali hiyo.Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti vya magurudumu vitatu ambavyo vitasaidia kubebea wagonjwa,Bandeji za kufungia vidonda,Ndoo za kuwekea taka,na vinginevyo.
 Hivi ni viti Vitatu vya kubebea wagonjwa ambavyo vilitolewa kama msaada kwenye Hospitali ya Palestina(sinza) na Farida Foundation.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Akimshukuru Bi Farida Abdul kwa kutoa msaada katika hospitali hiyo na akampongeza kwa moyo wake na kumsisitiza aendelee Kusaidia kila mara anapopata nafasi ili huduma zao ziwe bora zaidi kila siku.
 Mkurugenzi wa Farida Foundation Bi Farida Abdul akiongea na vyombo vya habari na kuelezea ni kwanini ameamua kutoa misaada hiyo katika hospitali ya Palestina,Amesema kwamba Serikali peke yake haiwezi kufika kwa kila mgonjwa na hospitali kwa wakati,kwa hiyo inatakiwa kujitoa kwa mashirika kusaidiana na Serikali ili Hospitalietu Ziweze kuwa na Huduma bora.
Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle ameishukuru Taasisi ya Farida Foundation kwa misaada waliyotoa kwani itawasaidia sana kuboresha Huduma zao.

BAADA YA KUTOKA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA FARIDA FOUNDATION WALIELEKEA UBUNGO DARAJANI KWA AJILI YA KUTOA MSAADA KWA MLEMAVU WA MIGUU,AMBAPO WALIMPATIA BAISKELI NA MTAJI WA VITU VYA BIASHARA
 Mkurugenzi wa Farida Foundation Bi Faridah Abdul akiongea na mlemavu wa miguu ndugu Marcerine Mayemba eneo la ubungo darajani kabla ya kumkabidhi msaada wa mtaji wa biashara pamoja na baiskeli atakayokuwa anaitumia.
 Bi Farida Abdul Akiwa na baiskeli ambayo aliikabidhi kwa mlemavu wa miguu bwana Marceline Mayemba,kwa ajili ya kumsaidia katika matumizi yake ya kila siku
 Mlemavu wa Miguu Bwana Marceline Mayemba Akipanda kwenye Baiskeli yake aliyokabidhhiwa na Farida Foundation
 Mlemavu wa Miguu Bwana Marceline Mayemba Akiendesha Baiskeli yake mara tu baada ya kukabidhiwa na Farida Foundation
 Bi Farida Abdul Akimkabidhi Mlemavu wa miguu bwana Marceline Mayemba Katoni ya Bidhaa ambazo ataanza nazo kama mtaji wa bishara,pia alikabidhiwa katoni tatu za maji,Katoni tatu za Juice na Katoni zingine Vifaa kama pipi,bigijii ili viwe kama kianzio kwa biashara yake.
Bi Farida Abdul Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi Mlemavu mwingine Chakula Pamoja na vinywaji.
ยช