Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
ambaye pia ni mkuu wa wilaya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanzishwa kwa mfuko
wa kuwasaidia wafanyabiashara wa soko la Mchikichini walioathiriwa na
janga la moto kwa lengo la kurejesha hali ya maisha waliyokuwa nayo hapo
awali.
Mmoja wa waanzilishi wa mfuko wa
kuwasaidia waathirika wa moto soko la Mchikichini ambaye pia ni Meneja
wa Vituo vya mizigo vya nchi kavu wa Kampuni ya AZAM Bw. Raymond Adolph
akieleza namna walivyoguswa na tukio la moto lililotokea katika soko
hilo na kuwaomba watanzania kuunga mkono juhudi hizo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa
soko la Mchikichini Bw. Jumanne Kongolo akiongea na waandishi wa
habari kuishukuru serikali na wananchi waliojitokeza kufungua mfuko wa
kuwasaidia waathirika wa moto katika soko hilo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko
la Mchikichini walioathiriwa na janga la moto wakifuatilia masuala
mbalimbali ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakati wa uzinduzi
wa mfuko wa kuwasaidia wafanyabiashara hao.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
---
Na Aron Msigwa – MAELEZO, Dar es salaam.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamejitokeza
kuanzisha mfuko maaluum wa kuwasaidia wafanyabiashara wapatao 5700 wa
soko la Mchikichini walioathiriwa na janga la moto lililotokea usiku wa
kuamkia tarehe 12 mwezi huu eneo la Karume,jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269