Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi
kwa jumla kuwa kutokana na kutetereka kwa daraja la reli kati ya
stesheni ya Ruvu na mchepuko wa reli ya Ruvu kwenda Mruazi usiku wa
kuamkia leo, umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi
ukarabati wa daraja utakapokamilika.
Tokea
asubuhi ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
na Wahandisi waandamizi na Mafundi ujenzi walifika katika daraja hilo
lililopo km 82/5 na kulifanyia tathmini kuwa linahitaji kuimarishwa ili
lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.
Kwa
taarifa hii wananchi na wateja wa TRL na wananchi kwa jumla ambao
walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya leo Juni 10, 2014 wanatakiwa
kufika katika stesheni zilizokaribu nao ili warejeshewe nauli zao ili
watafute usafiri mbadala.
Aidha Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam
Juni 10, 2014
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269