Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wa Mkoa
wa Dar es Salaam akiwemo Katibu Tawala Ndugu Theresia Mbando (wa tatu
kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (wa nne) nje
ya jengo la Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kupokea maandamano ya
wanafunzi wa shule za msingi za Dar es Salaam wakati wa sherehe ya
uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa huo tarehe
12.6.2014.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam wakiwa wamebeba
mabango yenye picha na ujumbe mbalimbali wakati wa sherehe za uzinduzi
wa Tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar zilizofanyika kwenye ukumbi
wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mchezo wa sarakasi iliyokuwa
ikichezwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar wakati wa sherehe
ya uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu
Raymond Mushi (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya E & D,
Ndugu Demere Kitunga (kushoto) wakati wakielekea kwenye ukumbi kwa ajili
ya sherehe za uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar
tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu
Theresia Mbando mara baada ya kuzindua rasmi Tamasha la vitabu vya
watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
terehe 12.6.2014.
Baadhi
ya watoto walioshiriki uzinduzi wa tamasha la vitabu mkoani Dar es
Salaam wakiwa wanasoma baadhi ya vitabu na majarida ya watoto wakati wa
sherehe hizo kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha moja ya kijarida cha hadithi kwa
ajili ya watoto alichokichagua kwa ajili ya kuwasomea hadithi watoto
wakati akizindua rasmi Tamasha la vitabu vya watoto kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa hapa Dar Es Salaam tarehe 12.6.2014.
Mgeni
Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu kwa wanafunzi wa
Shule za Msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mama Salma Kikwete
akiongea na wanafunzi wakati wa uzinduzi huo kwenye ukumbi wa Makumbusho
terehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mtoto Edda Kasika kutoka Shule ya
Msingi Maktaba tuzo kwa kushika nafasi ya pili katika uandishi wa insha
katika Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha la
vitabu kwa watoto tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
washindi wa insha na mchapishaji wa vitabu bora vya watoto na wageni
waalikwa mara baada ya kuzindua rasmi tamasha la vitabu vya watoto wa
shule tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia maonyesho ya vitabu, vijarida na
kazi mbalimbali zilizokuwa zikionyeshwa na wanafunzi wa shule za msingi
mkoani Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu
vya watoto tarehe 12.7.2014.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269