Mwenyekiti
wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa
Vijijini,Seleman Kiponda akikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu wa CCM
mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM
makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa.
Mwenyekiti
wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa
Vijijini,Seleman Kiponda akikabidhi bendera ya Chadema kwa Katibu wa
CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM
makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa.
Mwenyekiti
wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa
Vijijini,Seleman Kiponda akizungumza nia yake ya kuhamia CCM.
diwani wa kata ya Ihimbo Hezron Nganyagwa akimkabidhi bendera ya CCM aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema kata ya Ihimbo katika jimbo la Kilolo Selemani Kipondi.
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akizungumza wakati wa kumkaribisha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo,Seleman Kiponda baada ya kuhamia CCM katika ofisi za ccm mkoa wa Iringa.
Na Denis Mlowe, Iringa
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ihimbo jimbo la
Kilolo mkoani Iringa,Selemani Kiponda ameamua kuachana na chama hicho
na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukosa ushirikiano na
uongozi wa juu.
Kiponda
alifikia uamuzi huo juzi kwa kile alichosema amekuwa kiongozi
wa chadema kwa miaka minne na ameweza kushawishi wakazi wengi katika
maeneo mbalimbali katika kata ya Ihimbo kujiunga na chama hicho lakini
hawajawahi kupata ushirikiano kutoka uongozi wa juu wa chama wa mkoa
hadi taifa.
“Nilijiunga
na Chadema mwaka 1993 wakati ndio kwanza upinzani umeingia nchini na
nimekuwa kiongozi kwa miaka zaidi ya minne lakini hakuna ushirikiano
kutoka uongozi wangu hivyo nimerudi ccm kwa kuwa ndio chama changu
ambacho kwa kweli nilikuwapo tangu enzi za Tanu na hivyo kwa hiari yangu
nimeamua kurudi ndani ya chama makini na chenye sera zenye kueleweka”
alisema Kiponda”
Aidha
alisema kuwa hatua ya yeye kurudi CCM imetokana na maendeleo
yanayofanywa na diwani wa kata hiyo Hezron Nganyagwa pamoja na mbunge wa
jimbo la kilolo profesa Peter Msola kwa kuwa ushirikiano umekuwa mkubwa
kuliko ambavyo sikutegemea uwepo kwa kuwa nilikuwa chama cha upinzani.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema
Kiponda amefanya maamuzi sahihi ya kurudi CCM kwa kuwa muda mrefu
amekuwa Chadema hivyo ameona tofauti iliyoko miongoni mwa vyam hivyo
pinzani.
Mtenga
alisema kuwa viongozi na wanachama wa CCM wataendeleza ushirikiano
katika kuwarudisha wanachama wa Chadema wengine waliobaki Ihimbo kwa
kuwa kimefanikiwa kuwaunganisha wananchi katika kujiletea maendeleo
kutokana na uongozi imara wa chama hicho.
Naye
diwani wa kata ya Ihimbo Hezron Nganyagwa aliahidi kutoa ushirikiano
katika shughuli za maendeleo kama ilivyokuwa mwanzo walipokuwa
wakishirikiana ingawa walikuwa wapinzani.
Kurudi
kwa kiongozi huyo kunaongeza idadi ya wanachama wanne waliohama
Chadema hadi sasa wakiwemo Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini,
Emannuel Ngwalanje, Zawadi Waziri Shombe ambaye alikuwa ni mjumbe wa
oparesheni ya M4C Nyanda za Juu Kusini, pamoja na Bernado Lugenge.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269