Breaking News

Your Ad Spot

Jun 12, 2014

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MATHIAS CHIKAWE, IGP MANGU (KUSHOTO) NA KAMISHNA MKUU UHAMIAJI WAKIWA ZIARANI CHINA


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu (kushoto), Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile (wanne kushoto) wakipokea taarifa kuhusu Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mienendo ya Watu (Public Surveilance Sytem (Global eye) kutoka kwa Mtaalam wa Kampuni ya Telecom ya nchini China. Waziri Chikawe na ujumbe wake wapo jijini Beijing, China kwa ziara ya kikazi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma ya Mawasiliano nchini China, Li Ping alipokuwa akimfafanulia masuala mbalimbali ya mawasiliano yanayofanywa na Kampuni yake. Waziri Chikawe yupo jijini Beijing nchini humo na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile kwa ajili ya ziara ya kikazi.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma ya Mawasiliano nchini China, Li Ping. Waziri Chikawe na ujumbe wake wapo jijini Beijing, China kwa ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages