Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha
Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema
waliingia kituo kidogo cha Polisi cha Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa
na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu
wanaohitaji msaada.
Cha
kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika
kwa jina la Joseph Ngonyani na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye
kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30.
Ndipo
walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora
SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41
na kutoweka kusikojulikana.
Askari
Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali
ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye Venance amejeruhiwa
mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa
kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa
mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye Veronica Musime, askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo
Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
CHANZO:Michuzi Blog
Rip kamanda
ReplyDelete