Breaking News

Your Ad Spot

Jun 14, 2014

PICHA:MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AWASILI KIGOMA AKIWA MGENI RASMI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA UCHANGIAJI DAMU SALAMA KITAIFA.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mtoto Mosi Kimosa ,7, anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Msimba iliyoko Kigoma Vijijini na Trisa Luziga,6, anayesoma darasa la kwanza mara baada ya Mama Salma kutua katika uwanja wa ndege wa Kigoma
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Issa Machibya akimpokea rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma Mama Salma yuko mkoani humo kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Kigoma leo
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma za utamaduni zilizokuwa zikichezwa na akinamama wa Kigoma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kushiriki maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani humo leo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages