Breaking News

Your Ad Spot

Jun 8, 2014

TWITTER YATHIBITISHA RASMI AKAUNTI YA DIAMOND NA VANESSA MDEE

Diamond & Vee MoneyKwa wale watumiaji wa mtandao maarufu wa kijamii wa Twitter, bila shaka hawatakuwa wageni wa zile akaunti ambazo zinakuwa zimethibitishwa rasmi au kwa jina lingine Verified Account ambazo kwa kiasi kubwa humilikiwa na watu mashuhuri kama vile  marais, wasanii wa muziki, filamu na wanasiasa.
Kwa hapa kwetu Tanzania ni baadhi ya watu wachache waliobahatika kumiliki akaunti za namna hiyo akiwemo  mkuu wa nchi Rais Jakaya Kikwete,  mbunge wa Bumbuli kupitia tiketi ya CCM Mhe.january Makamba pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya  AY.
hata hivyo idadi hiyo imeongezeka tena baada ya wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya wanaofanya vizuri katika gemu, hapa namzungumzia mshindi wa Tuzo saba za Kili Diamond Platnumz na Vanessa Mdee baada ya akaunti zao za Twitter  kuwa Verified.
”What a birthday just got verified!!! Heeeey @Verified that’s wussup” aliandika Vanessa AKA Vee Money ambaye leo anasherekea siku yake ya kuzaliwa na kwa upande wa Diamond nae hakuwa nyuma aliandika  ”Thank You Twitter”
Diamond Platnumz Vee Money

Happy BornDay Vee Money!!!

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages