Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo akiwaongoza
washindi wa tiketi ya Winda SAFARI YA Brazil na Serengeti mara baada ya
kuwasili katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere. Nyuma ni Bi
Juliana Joseph Masawe(mshindi)
Mshindi
wa tiketi ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti Deusdedit Kahwa kutoka
Dar es Salaam akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara
baada ya kuwasili nchini huku akiahidi kushiriki katika kila promosheni
zitakazokuwa zikichezeshwa na kampuni ya SBL.
Menrad
Faustin Shayo kutoka Arusha akihojiwa na waandishi mara baada ya
kurejea nchini. Bw. Shayo alielekea nchini Brazil baada ya kushinda
tiketi kupitia kampuni ya bia ya Serengeti. Shayo aliambatana na
washindi wawili katika ziara ya utembelea vivutio mbalimbali.
Bi
Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro akieleza kwa kufuraha juu ya
mambo mazuri aliyoyaona nchini Brazil huku akiwashukuru kampuni ya bia
ya Serengeti kwa kumwezesha kula bata kiasi ambacho hakutegemea maishani
mwake.
Pilikapilika
za washindi mara baada ya kuwasili nchini kutokea Brazil kula bata
baada ya ushindi kupitia kampeni ya Winda Tiketi ya Brazil na Serengeti
iliyokuwa ikichezeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake
ya Serengeti Lager. Kulia ni Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam, Bi
Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro (katikati) pamoja na kushoto ni
mwenyeji wa washindi hao Bw. Allan Chonjo Meneja Masoko wa kampuni ya
Serengeti.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269