Breaking News

Your Ad Spot

Sep 16, 2014

KINANA AWASILI MAFIA KWA BOTI, ALAKIWA NA MAMIA YA WANANCHI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda boti kutoka Nyamisati wilayani Rufiji kwenda wilayani Mafia kuendelea na ziara yake katika mkoa wa Pwani, leo Septemba 16, 2014
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipanda boti kutoka  kutoka Nyamisati wilayani Rufiji kwenda wilayani Mafia kuendelea na ziara ya Kinana katika mkoa wa Pwani, leo Septemba 16, 2014
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisafiri na wananchi katika boti kutoka Nyamisati kwenda Rufiji katika mkoa wa Pwani leo.
 Wananchi wa Mafia wakiwa wamekusanyika kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi, kumlaki Kinana alipowasili leo Kisiwani Mafia mkoani Pwani leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili Mafia leo. Mbele yake ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Kinana akiwasalimia wananchi waliofika kumlaki Mafia
 Mwandishi wa Habari Leo Anastazia Anyamike akishuka kwenye boti Mafia baada ya kuwasili na Kinana
 Mwandishi wa Star Tv, Joseph Mpangala akishuka kwenye boti na vifaa vyake vya kazi baada ya kuwasili na Kinana kisiwani Mafia
 Mpigapicha Mkuu wa Jamboleo Richard Mwaikenda ambaye  pia mtayarishaji wa Kamanda wa Matukio Blog akishuka kwenye boti katika msafara huo
Mwandishi wa Jamboleo, Said Mwinshehe akishuka kwenye mtumbwi baada ya kuwasili na Kinana katika kisiwa cha Mafia leo
Waandishi wa habari wakipelekwa kwa boti dogo ufukweni baada ya kuwasili kwa boti kwenye pwani ya Kisiwa cha Mafia, leo. Picha zote na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages