Mkazi mmoja wa
kitongoji cha Jangwani mjini Sumbawanga akihama kwa kutumia mkokoteni kutoka
eneo moja kuelekea jingine kama alivyonaswa na mpigapicha wetu
Baadhi ya madereva wa pikipiki maarufu kama boda doda wakiwa katika foleni ya
kusubiri mafuta katika kituo kimoja kinachouza bidhaa hiyo, mafuta aina ya
petroli yameadimika mjini Sumbawanga baada ya juzi mamlaka ya kudhibiti bei ya
nishati na maji kutangaza kushuka kwa bei ya mafuta kutoka Sh 2500 hadi 2100.
Baadhi ya abiria wakiwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Land Cruser jana
wakifanya safari kati ya Sumbawanga mjini kuelekea Bonde la Ziwa Rukwa, hali
hiyo ni hatari kwa watu na mizigo lakini inajitokeza kutokana na ugumu wa
usafiri katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269