Breaking News

Your Ad Spot

Mar 11, 2015

UONGOZI WA SERIKALI WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA , WAMEDHAMIRIA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WENYEVITI WA SERIKALI ZA JIJIJI NA MITAA WILAYANI HUMO

 Na  Walter  Mguluchuma
Nkasi

UONGOZI wa Serikali wilayani Nkasi mkoani Rukwa, umedhamiria kuwafikisha mahakamani wenyeviti wa serikali za vijiji na mitaa wilayani humo, wanaohamasisha wananchi wasichangie ujenzi wa majengo ya maabara katika shule za sekondari.

Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Iddy Kimanta alisema hayo juzi wakati wa katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Nkasi kilichofanyika katika ukumbi wa Community Center uliopo wilayani humo.

Alisema kuwa wapo baadhi ya wenyeviti wa vijiji na mitaa wamekuwa wakihamasisha wananchi kutochangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya maabara katika shule za sekondari za kata, "huku wakijinadi kwamba wao ndio serikali"hali ambayo imechangia kutokamilika kwa majengo mengi ya maabara katika shule hizo.

"Mie nawashangaa sana......wanathubutu kutamba kwamba wao ndio serikali na wanawazuia wananchi wasichangie michango kwa ajili ya ujenzi wa maabara......sheria ipo wazi kwa mtu anayekaidi maagizo ya viongozi wake sasa nataka kuona inachukua mkondo wake, tayari nimezungumza na polisi na mahakimu" alisema mkuu huyo wa wilaya.

Aliongeza kuwa ujenzi wa maabara ni kwa manufaa ya wananchi wote hususani wakazi wa wilaya hiyo ambayo watoto wao ndio watakaonufaika pindi maabara hizo zitakapokamilika na kuwa na vifaa vyote kama ambavyo serikali imedhamiria.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kujali itikadi za watu kisiasa, yeye jukumu lake ni kuhakikisha hamashauri hiyo inapata maendeleo endelevu katika sekta zote ikiwemo elimu, hivyo atahakikisha wote wanachangia michango na atakayekaidi sheria itachukua mkondo wake.

Kwa mujibu wa MKurugenzi wa halmashauri hiyo, Kimulika Galikunga ujenzi wa majengo hayo unakwenda vizuri na halmashauri imechangia kiasi cha Sh 140 milioni ili kufanikisha ukamilikaji wake

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages