Breaking News

Your Ad Spot

Apr 15, 2015

CHIKAWE, ASASI KIRAIA ZINAZOJIHUSISHA NA SIASA KUFUTWA


Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa Habari ( hawapo pichani) kuhusiana na Taasisi za Dini na vikundi mbalimbali kuepuka kushiriki katika vitendo ambavyo vinaashilia kuvuruga amani na utulivu nchini jijini Dar leo.

Baadhi ya Waandishi habari waliohudhuria katika mkutano wa wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es salaam leo.Picha Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii. 
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
ASASI za Kiraia zilizosajiliwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,vinavyojihusisha na siasa na kuacha katiba zao vitaanza kufutwa kuanzia Aprili 30 mwaka huu.
Hayo ameyasema Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika Kura ya maoni pamoja na Uchaguzi Mkuu,Chikawe amesema serikali iko imara katika kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani hivyo watu wanaotaka kuharibu amani kutumia asasi za kiraia na kuacha katiba zao watafutwa.
Chikawe amesema katika kuelekea uchaguzi kumekuwa na asasi za kiraia zikijihusisha na siasa kwa kuchangisha fedha kwa ajili kuwashawishi viongozi wa siasa wagombee hiyo ni kwenda kinyume na katiba zao na kutakiwa kufutiwa usajili.
Amesema katika suala la ugaidi ni tatizo la dunia hivyo kinachofanyika ni kuimarisha ulinzi katika maeneo yetu na kupata taarifa kwa watu wanaoingia nchini na watu wanaobainika kutoa kuwa na taarifa wanawarudisha katika nchi zao.
Chikawe amesema vijana wa kitanzania ambao wamekamatwa nchini Kenya kuhusika na ugaidi hawana taarifa, wanachokifanya ni kupata taarifa kutoka Kenya kama kuna watu wengine wapo katika kundi la al-shabab.
Aidha amesema jeshi liko imara hivyo wananchi waishi kwa amani kwani serikali ina imarisha ulinzi kuhakikisha amani inakuwepo. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages