Taarifa zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde kutoka chanzo cha kuaminika,zinaeleza kuwa Basi la kampuni ya Gamet Trans linalofanya safari zake Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea limepata ajali maeneo ya Kibiti wilaya ya Rufiji-Utete mkoa wa Pwani baada ya kutaka kumkwepa mtu anayedaiwa kuwa na tatizo la ulemavu wa akili,lakini kwa bahati mbaya likamgonga na kufariki papo hapo,taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya ajali hiyo basi hilo liliacha njia na kupinduka na kupelekea kifo cha mtu mmoja aliyegongwa na wengine waliokuwemo ndani ya basi hilo (idadi ya abiria haikujulikana mara moja) kujeruhiwa.
Basi la kampuni ya Gamet Trans linalofanya safari zake Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea lilipinduka watu wakiwa wanajaribu kuokolewa.
Basi la kampuni ya Gamet Trans linalofanya safari zake Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269