Waasi Mashariki mwa Urain
Mawaziri
wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani , Ufaransa , Urusi na Ukrain
wameelezea wasi wasi uliopo kufuatia kutokea kwa mapigano mashariki mwa
ukrain na kikiukwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa
mwezi Februari.
Baada ya
mazungumzo yaliyofanyika mjini Berlin waziri wa mashauri ya kigeni wa
Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari kuwa
kati ya silaha ambazo zitaondoa ni pamoja na vifaru.
Pande
hizo mbili zilionekana kuheshimu makubaliano hayo hadi kulipotokea
mapigano ya hivi majuzi kwenye uwanja wa ndege wa Donetsk na kijiji cha
Shyrokyne nje ya mji wa Mariupol.
Pande hizo pia zimekubaliana kuendelea kubadilishana wafungwa.(Muro)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269