- Wanaotaka urais kujulikana Juni
- Wakiuka sheria kukiona
- Mbwembwe marufuku
Hata hivyo, chama hicho kinatarajia kubadilisha baadhi ya taratibu za mchakato mzima wa uchukuaji wa fomu hizo tofauti na ilivyokuwa wakati wa kutafuta mgombea wa chama hicho mwaka 2015.
Vyanzo vya kuaminika vya gazeti hili vimeeleza kwamba wanaotaka kuwania urais kupitia CCM wataanza kuchukua fomu zao mwanzoni mwa mwezi ujao kupitia utaratibu maalumu utakaotangazwa.
"Chama kitaruhusu wagombea kuchukua fomu katika wiki ya kwanza ya mwezi Juni mwaka huu kupitia utaratibu maalumu utakaotangazwa na chama wakati ukifika," kilieleza chanzo hicho kilicho karibu na uongozi wa juu wa CCM.
Tofauti na katika chaguzi za mwaka 1995 na 2005, safari hii CCM inaendesha mchakato wake wa kutafuta wagombea katika hali ya usiri mkubwa, huku ikielezwa kwamba chama hicho hakitaki kufanya makosa yatakayonufaisha vyama vya upinzani.(P.T)
Gazeti
hili limeambiwa kwamba hivi sasa, CCM kinaandaa taratibu na kanuni
zitakazotumika katika mchakato huo na kwenye ngazi za ubunge na udiwani
ambazo katika baadhi ya mambo ni tofauti na zile zilizotumika mwaka
2005.
Kwa
mfano, Raia Mwema limeambiwa kwamba huenda chama kikaangalia upya
utaratibu wa kutafuta wadhamini mikoani tofauti na ule uliotumika mwaka
2005.
Mwaka 2005, waliokuwa wasaka urais kupitia CCM walilazimika kutafuta wadhamini katika mikoa tofauti ya Tanzania Bara na Zanzibar ili kuonyesha kuwa wanaungwa mkono na wanachama wa mikoa mbalimbali na pande zote mbili za Muungano.

Itakumbukwa
kwamba wakati huo, aliyekuwa mgombea mwenye nguvu ndani ya CCM, John
Cigweyemisi Malecela, alizunguka mikoani kwa ndege ya kukodi na kumaliza
zoezi hilo ndani ya wiki moja.
"Watu wengi hawafahamu lakini wakati tulipokuwa na mchakato kama huu mwaka 1995, haikuwa lazima kwa wagombea kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini. Tuliokuwa ndani ya chama wakati huo tukishuhudia kila kitu hili halikuwepo.

"Lakini
chama kikatumia utaratibu huo wa kutafuta wadhamini mwaka 2005 ambao
haukuwepo huko nyuma. Hivyo, mwaka huu, chama kinaweza kuona kuwa ni
busara kutoendelea na utaratibu kama huo,"
"Chama ni chombo kilicho dynamic (kinachobadilika). Hatuwezi tukaacha CCM iwe static (bwete). Kwa mfano, kama mwaka 1995 tulikataza watu wasiende mikoani ili kuzuia wasitoe rushwa, mwaka huu hali imebadilika. Si lazima mtu akutane na mtu ndiyo atoe rushwa. "Akiwa na simu yake ya mkononi anaweza kumpa rushwa yeyote amtakaye, popote pale alipo hapa nchini. Ndiyo maana chama hakiwezi kuwa na mawazo mgando. Ni lazima kanuni na taratibu zake ziakisi wakati husika," kilisema chanzo hicho cha Raia Mwema.

Raia
Mwema limeambiwa kwamba katika uchaguzi wa mwaka huu, wana CCM
wanatamani kuona kuwa watu wote wanaojitokeza kutaka kuwania nafasi hiyo
wanapata fursa sawa ya kuendesha shughuli zao.
"Kuna wagombea watakuwa na uwezo wa kuwa na ndege za kukodi na wengine hawatakuwa nao. Kuna wagombea wanaweza kuwa na msafara wa magari 100 na wengine mawili tu.
"Kuna wagombea watakuwa na uwezo wa kuwa na ndege za kukodi na wengine hawatakuwa nao. Kuna wagombea wanaweza kuwa na msafara wa magari 100 na wengine mawili tu.
"Kuna
wagombea wana nafasi kubwa serikalini ambazo zinawapasa kusindikizwa na
ving'ora na wana walinzi. Mwaka 2005, kama unakumbuka, aliyekuwa Waziri
Mkuu, Frederick Sumaye, alienda kuchukua fomu bila msafara. Tunataka
hali iwe hivyo pia safari hii.
"Mwaka
huu, sidhani kama chama kitakubali wagombea wengine waonekane wana faida
kuliko wenzao. Lengo ni kwamba, kila mgombea apate fursa sawia ya
kukutana na wanachama na kueleza yale aliyokusudia kuyafanya endapo
chama kitampitisha," mmoja wa wagombea aliyewania nafasi hiyo mwaka 2005
na ambaye anatajwa kutaka kuwania tena nafasi hiyo mwaka huu aliliambia
gazeti hili juzi Jumatatu.
Ubunge
Ubunge
Katika
hatua nyingine, gazeti hili linafahamu kwamba kuna uwezekano mkubwa
chama hicho kikabadili utaratibu wake wa kupata wagombea wa nafasi ya
ubunge kulinganisha na ule uliotumika mwaka 2005.
Wapo wana CCM wanaoamini kwamba chama chao kilipoteza baadhi ya viti vya ubunge mwaka 2005 kutokana na utaratibu mbovu wa kutafuta wabunge kupitia mtindo wa kura ya maoni.
Wapo wana CCM wanaoamini kwamba chama chao kilipoteza baadhi ya viti vya ubunge mwaka 2005 kutokana na utaratibu mbovu wa kutafuta wabunge kupitia mtindo wa kura ya maoni.
"Unakuta
kwenye jimbo moja chama kina watu 20 wanaotafuta nafasi moja tu ya
ubunge. Utaratibu uliotumika mwaka 2005 ulikuwa kwamba wote hao
wanakwenda kupigiwa kura na wana CCM kwenye majimbo yao jambo ambalo
lilileta matatizo mengi.
"Kuna watu ndani ya chama wanaamini kwamba inatakiwa vyombo vya chama vifanye kazi yake kiasi kwamba majina yanayokwenda kwenye kura ya maoni yasizidi matatu. Na hao watatu ni lazima wawe wale ambao wamefuata taratibu zote za chama.

"Hili
litazuia watu kutoa rushwa mapema na hovyo hovyo. Maana, kama mko watu
20, nani atatoa rushwa wakati akijua wanatakiwa watu watatu tu na tena
waliofuata taratibu zote?" alisema mmoja wa waliokuwa viongozi wa CCM
Mkoa wa Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Akizungumza na Raia Mwema kuhusu kuthibitisha kuanza kwa mchakato huo mwezi ujao, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema chama kitatoa taarifa kuhusu jambo hilo wakati ukifika.
Akizungumza na Raia Mwema kuhusu kuthibitisha kuanza kwa mchakato huo mwezi ujao, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema chama kitatoa taarifa kuhusu jambo hilo wakati ukifika.
"Nimewahi
kusema huko nyuma na sijui kama mlinisikia kuwa CCM haitawahi wala
kuchelewa kwenye suala la uchaguzi wa mwaka huu. Wakati ambao tutaamua
kufanya mambo yetu utakuwa ndiyo wakati sahihi na wenyewe.
"Haya mambo yanakwenda kwa pamoja. Unaweza kufanya uamuzi sahihi ikiwa si kwa wakati, unaharibu. Uamuzi sahihi unaendana na wakati sahihi. Katika wakati sahihi ukifika, tutafanya uamuzi sahihi," alisema Nape.

Kuhusu
madai kwamba safari hii CCM imetawaliwa na usiri mkubwa katika mchakato
mzima wa uchaguzi, Nape alisema suala hilo si la kweli kwani
linavumishwa na watu wasiojua utendaji wa chama hicho.
Alisema mara nyingi ratiba ya uchaguzi ndani ya CCM hupangwa kuendana na ile inayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo hadi sasa haipo.
Alisema mara nyingi ratiba ya uchaguzi ndani ya CCM hupangwa kuendana na ile inayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo hadi sasa haipo.
Ingawa
hadi sasa chama hakijafungua rasmi milango kwa wagombea wake kujitangaza
na kupiga kampeni za waziwazi, tayari baadhi ya majina yamekuwa
yakitajwa mara kwa mara kuwa yataingia kwenye kinyang'anyiro cha
kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Miongoni mwa majina yanayotajwa kutoka ndani ya CCM ni Edward Lowassa, Bernard Membe, Mizengo Pinda, Profesa Mark Mwandosya, January Makamba, Frederick Sumaye, Steven Wasira, Dk. Asha Rose Migiro, Makongoro Nyerere na Dk. Hamis Kigwangala.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269