Maandamano nchini Burundi
Watu
wanne wamekufa na wengine tisa kujeruhiwa katika maandamano
yanayoendelea kupamba moto nchini Burundi kupinga hatua ya rais Pierre
Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Mwandishi
wa BBC aliyepo mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura anasema mamia ya watu
wamejitokea kwenye maandamano hayo huku baadhi wakichoma moto baadhi ya
vitu.
Siku ya
jumanne Mahakama ya Katiba ilikubali kuwa Rais Nkurunziza anaweza
kugombea urais ambapo ilisema ni halali yeye kuwania tena urais kwa
kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika
hotuba yake siku ya jumatano Rais Nkurunziza alisema kama atachaguliwa
tena kuongoza nchi hiyo, muhula huu utakuwa wa mwisho kwake kuwa
madarakani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269