Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri
mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amefikia mkataba wa kuunda serikali
mpya ya pamoja, muda mfupi kabla ya kumalizika kwa muda uliokuwa
umepangwa.
Makubaliano
yake na chama cha mrengo wa kulia cha Kiyahudi, Jewish Home Party
yanamhakikishia kupata wingi wa wabunge katika bunge la Israel, japo kwa
kiasi kidogo akiwa na viti 61 katika bunge la wajumbe 120.
Chama
hicho cha Kiyahudi kinachotetea upanuzi wa makazi ya Wayahudi katika
maeneo ya Wapalestina, kimepewa wizara muhimu ya Sheria. Muungano huo
pia unakihusisha chama cha ultra Orthodox.
Katika
mkutano wa waandishi wa habari, ukihudhuriwa na kiongozi wa chama cha
Kiyahudi, Naftali Bennett, Bwana Netanyahu amesema kazi kubwa katika
kuunda serikali ya pamoja.
Chama cha Bwana Netanyahu cha Likud kilishinda uchaguzi wa mwezi Marchi kwa kupata viti 30
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269