Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakivushwa kwenye mafuriko kwa kulipia sh. 2,000 maeneo ya Jangwani Dar es Salaam leo. Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ilifungwa kwa muda baada ya mafuriko hayo kufunika daraja. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA RICHARD MWAIKENDA NA KHAMISI MUSSA )
Kijana ambaye jina lake
halikupatikana mara moja akimbeba msichana na kumvusha kwenye mafuriko
kwa malipo ya Sh. 2,000 eneo la Jangwani Dar es Salaam leo.
Lori lililokuwa limebeba kokoto
likiwa limesombwa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili
jijini Dar es Salaam na kutumbukia kwenye Mto Msimbazi, karibu na daraja
la Kinyerezi jijini leo.
Wananchi wa Bonde la Mkwajuni
Barabara ya Kawawa wakiwa wamehifadhiwa jirani na nyumba ya Mjumbe Sofia
Philipo baada ya nyumba zao kujaa maji leo kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Nyumba zilizopo Bonde la Jangwani
karibu na Klabu ya Yanga, zikiwa zimezingirwa na maji ya mvua
iliyonyesha leo na kusababisha mafuruko.
Nyumba zilizopo Bonde la Jangwani
karibu na Klabu ya Yanga, zikiwa zimezingirwa na maji ya mvua
iliyonyesha leo na kusababisha mafuruko.
Kijana akiwa amebeba baiskeli yake
kwa ajili ya kujitayarisha kuvuka maji kwenye bonde la Msimbazi,
Barabara ya kuelekea Magomeni na Ubungo jijini Dar es Salaam.
Juu na chini: Baadhi ya wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam, wakivushwa kwenye mafuriko kwa kila mmoja kulipia
sh. 2,000 maeneo ya Jangwani Dar es Salaam leo. Barabara ya Morogoro
eneo la Jangwani ilifungwa kwa muda baada ya mafuriko hayo kufunika
daraja.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269