Mratibu
wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa Mama Ye unaoendeshwa na
asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
Uingereza (DFID), Chiku Lweno akielezea jitihada zinazofanywa na mradi
wa Mama Ye katika kukabiliana na vifo vya Mama na mtoto ambapo aliwataka
waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelemisha jamii ili iweze
kuepukana na vifo vya mama na mtoto ambalo nalo ni janga la taifa.(Picha
zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Musoma
SERIKALI
imeshauriwa kuhakikisha sera na mipango mizuri iliyopo kwa afya ya mama
na mtoto mchanga inasimamiwa na kutekelezwa ili kuliondoa taifa katika
janga la kupoteza mama na watoto wakati wa uzazi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa
Mama ye unaoendeshwa na asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Chiku Lweno katika mafunzo
kwa waandishi wa habari mjini Musoma.
Alisema
bila kutekeleza mipango mizuri ambayo Rais Jakaya Kikwete amekuwa
championi wa masuala ya wanawake na watoto kitaifa na mataifa, tatizo la
vifo kwa wanawake wenye pingamizi za uzazi na watoto wachanga.
Alisema
kutokana na haja ya kutoa msukumo katika masuala ya uzazi wameamua
kuwapatia elimu waandishi wa habari ili wawe chachu ya kutambua umuhimu
wa ukunga na uzazi salama.
"Tunafunza
waandishi wa habari ili waweze kusukuma mbele shahuri hili ili kila
mtu katika nafasi yake atetee nafasi yake" alisema Lweno.
Alisema
suala la mama na mtoto mchanga ni masuala mtambuka ambapo mambo mengi
lazima yaunganishwe yafikiriwe na kutambuliwa ili kudhibiti vifo vya
wanawake na watoto wachanga.
Alitaja
masuala hayo kama upangaji wa bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kusaidia
kupatikana kwa wakunga wataalamu na vifaa vyao vya kazi na maeneo ya
kufanyia kazi. Aidha kuwapo kwa ukubali wa wakunga na elimu ya uzazi.
Alisema
ni vyema waandishi wa habari kama watia chachu kuelimishwa mambo mengi
yanayohusiana na uzazi salama ambapo ndani yake kuna masuala ya bajeti
na ufuaji wa wataalamu na ufuatuiliaji wa sera na sheria zilizopo katika
kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.
Alisema anaamini waandishi wa habari wakielewa mambo hayo watasaidia kukomaa nalo na kuwezesha kila mtu kuwajibika.
Kaimu
Muuguzi Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.
Ama Kasangala akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo ya siku moja
yaliyofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA)
kuelekea kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga
duniani ambapo kitaifa imefanyika mkoani Mara.
Naye
Afisa Muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii,
Saturini Manangwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari alisisitiza
haja za waandishi kutambua dhana ya afya ya mama na mtoto kuwa ni kitu
mtambuka kutokana na suala la lenyewe kutegemeana.
Alisema
serikali inapohimizwa kuwekeza kwa mkunga kunatokana na ukweli kuwa
huduma ya mama na mtoto mchanga itakujwa bora kwa kuwa na mkunga bora
mwenye vifaa na anayefahamu wajibu wake kuanzia ujauzito wa mama hadi
kujifungua kwake.
Alisema
uwekezaji huo unagusia changamoto nyingi zilizopo sasa kama upungufu
wa wakunga, vituo vya kutolea huduma, dawa, miundombinu na masuala anuai
ambayo yameegemezwa na utambuzi wa bajeti na umuhimu wake kama
kipaumbele.
Alisema kwamba katika upangaji bajeti kila kitu kinategemea huwezi kusema unazidisha hiki na unakiacha hiki.
Alisema
mathalani katika hali bora ya ukunga na uwezo wa kumsaidia mhusika
,viwango vya dunia vilivyoweka na Shirika la Afya Duniani (WHO) kila
mkunga mmoja ahudumie angalau watu sita, lakini sehemu kubwa ya dunia
haifikii hivyo.
Aidha
alisema kwa Tanzania kiwango ni mkunga mmoja ahudumie watu 20-25 lakini
kwa sasa Tanzania mkunga mmoja anahudumia zaidi ya watu 50.
Kimsingi
alisema Tanzania ina tatizo la wakunga na pamoja na serikali kuanzisha
vyuo vya kufunza wakunga na kukubali mashirika ya dini nayo kufanya
hivyo hali bado ni tete.
Hata hivyo alisema ni kupitia wakunga waliowataalamu upo uwezekano wa kuzuia vifo visivyo vya lazima.
Mratibu
wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy akizungumzia nia ya
chama hicho ni kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa
anapata huduma za mkunga mtaalamu.
Muuguzi
huyo mwandamizi pia alisema katika juhudi za serikali kunaanzishwa
mafunzo ya mwaka mmoja ambapo yatatoa maofisa afya ambao kazi yao kubwa
itakuwa kujua idadi ya wanawake wajawazito na wagonjwa katika maeneo yao
na kutoa taarifa kwa zahanati iliyo karibu.
Alisema
ofisa huyo kazi yake haitakuwa hospitalini au kwenye zahanati bali
kwenye jamii akitambua idadi ya wagonjwa wake na kutoa taarifa sahihi ya
hali ya afya ya kitongoji chake kwenye zahanati.
Mmoja
wa washiriki Belina Nyakeke ambaye ni mwandishi wa habari wa magazeti
alisema kwamba amefurahishwa na mafunzo hayo ambayo yamempa nafasi ya
kutambua wajibu wake katika kusaidia kuondoa tatizo la vifo vya mama na
mtoto mchanga.
Alisema japokuwa mafunzo ni ya muda mfupi lakini yamemfumbua macho kutambua wajibu na haki kwa wananchi na serikali.
Naye
Ahmed Makongo akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemfanya atambue
wajibu wake kusaidia kusukuma mambo yaende sawa kwa upande wa waamuzi na
pia wananchi husika kwa kuzingatia mafunzo hayo yaliyoletwa kwao na
Mama Ye na UTTPC chini ya Ufadhili wa Shirika la Mpango wa watu Duniani
(UNFPA).
Ofisa
muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini
Manangwa akizungumza changamoto za upungufu wa wakunga, vituo vya
kutolea huduma, dawa, miundombinu n.k wakati wa mafunzo kwa waandishi wa
habari wa mjini Musoma mkoani Mara.
Ofisa
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) anayeshugulikia
mifumo ya Afya, Felista Bwana akitoa takwimu za nchi zinazoongoza kwa
vifo vya mama na mtoto kwenye mafunzo ya waandishi wa habari mjini
Musoma.
Mwandishi
wa habari wa gazeti la The Citizen, mkoani Mara, Belina Nyakeke
(katikati) akishiriki kwenye mafunzo ya waandishi wa habari
yaliyofanyika mjini Musoma na kufadhiliwa na Shirika la UNFPA.
Mwandishi
wa habari wa gazeti la Tanzania Daima mjini Musoma, Igenga Mtatiro
akiuliza swali kwa Afisa muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Saturini Manangwa (hayupo pichani).
Pichani
juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Mara ambao pia
wanachama wa vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) walioshiriki
mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mradi wa Mama Ye kwa kushirikiana na
UTPC na kufadhiliwa na UNFPA.
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Rais
wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya
(kushoto), akibadilishana mawazo na Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini
(TAMA), Martha Rimoy mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid afungua semina ya Waandishi wa Habari kuhusu Usalama wa Chakula katika kuadhimisha Siku ya Afya Duniani jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kushoto), akihutubia
wakati akiifungua semina ya siku moja ya waandishi wa habari kuhusu
usalama wa Chakula katika kuadhimisha Siku ya Afya Duniani, jijini Dar
es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani
(WHO), nchini Tanzania, Dk. Rufaro Chatora.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk. Rufaro Chatora
akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando (kushoto), akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando (kulia),
akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kinga ... wa wizara hiyo, Dk.Georgina Msemo
wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Mkurugenzi
wa Usalama wa Chakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Raymond
Wigenge (kushoto), akielekezana jambo na Ofisa Afya Muelimishaji wa
Wizara hiyo, Aggrey Mshana wakati wa Semina hiyo.
(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
Uzinduzi wa Huduma Mpya ya MaxMalipo kwa kutumia Simu ya Kiganjani
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa kampuni ya
MaxCom Africa Bw. Deogratius Lazari akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu Huduma Mpya ya MaxMalipo kwa kutumia simu ya kiganjani ijulikanayo kama
SmartMalipo. Kushoto ni Afisa wa MaxCom Bw. Geofrey Mwakamyanda na kulia ni
Meneja wa MaxCom Kanda ya Mashariki Bw. Thomas Mwakalindile. (Picha na Idara ya Habari-Maelezo)
MAXCOM Africa maarufu kama MaxMalipo ni kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010
ambayo imewekeza katika kurahisisha maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla
kiuchumi na kijamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano (ICT
Technology)
Ili
kufikia malengo na Sera ya Taifa ya kutumia mifumo ya kielekroniki kutoa huduma
na pia kuwezesha Watanzania walio wengi kufikiwa na huduma hizi (Financial
Inclusion) na pia kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza
ajira, MaxMalipo imeanzisha huduma mpya
itakayomuwezesha mtanzania kulipa bili zote kwa kutumia simu ya kiganjani aina ya
Smart phone yenye Mfumo utakaojulikana kama SmartMalipo.
Huduma
hii
inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania takribani laki mbili (200,000)
nchi nzima kufikia mwaka 2016 na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta isiyo
rasmi ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi.
Mfumo huu utaweza kurahisisha ulipaji wa bili mbalimbali Mfano; Umeme
(Luku), Ving’amuzi vya Televisheni, Vocha za Mitandao yote, Kulipia Kodi
za TRA
na Baadae Kufanya Miamala ya Kibenki
inayohusisha Kuweka na Kutoa fedha, huduma ambazo kwa sasa zinalipwa
kupitia mashine za MaxMalipo.
Huduma
hiyo inapatikana kwenye mfumo wa simu ya kiganjani ambapo mtumiaji atalazimika
kuweka mfumo wa SmartMalipo (Download
Smart Wakala Application) kutoka tovuti ya Google play au tovuti ya Maxmalipo
kwa kuandika neno ‘SmartMalipo au Maxmalipo’. Kisha mtumiaji atapata
maelekezo ya jinsi ya ku-install mfumo huu
kwenye simu yake na jinsi ya kutumia. Mfumo huu utamwezesha mtumiaji yeyote
kuwa Wakala na kulipia huduma zilizo orodheshwa.
Mtumiaji wa
mfumo huu atajipatia kamisheni
kama alivyo wakala mwingine wa Maxmalipo kwa Huduma atakazofanya.
Watumiaji
wa mfumo huu wa SmartMalipo watatambulika kwa jina la ‘Smart Wakala’ popote
walipo na kufanya biashara kupitia simu zao za kiganjani.
MaxMalipo
imeanzisha huduma hii mpya kwa lengo la kuwawezesha watanzania walio wengi
kufikiwa zaidi na huduma za malipo kwa
haraka wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wenye mitaji midogo ambao kwa mazingira yao ni vigumu kuwa na
Mashine za Maxmalipo.
MaxMalipo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kupunguza matatizo ya foleni kwenye malipo ya huduma mbalimbali kama bili za
TRA, LUKU, DAWASCO, huduma za kibenki na hata katika mifuko ya Hifadhi ya jamii
Mfano PSPF.
Mwisho
kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo inatoa rai kwa watanzania hasa
wafanyabiashara kuchangamkia huduma
zinazotolewa na kampuni hii ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia
katika mifumo ya utoaji huduma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269