Kashikashi za kuambiwa umefumaniwa zisikie kwa mwenzako tu! Utakuta mtu mkubwa, bonge, lakini akidaiwa amefumaniwa, nguvu zote zinakwisha! Sijui kwa nini?!
Mfanyabiashara
mmoja wa jijini Arusha ‘pedeshee’ aliyejulikana kwa jina la Aldina
Hashim, mkazi wa Unga Limted, amechezea kichapo baada ya rafiki yake
kipenzi, Emmanuel Mwambije kudai amemfumania na mke wake, Felista
Mwambije.
Kwa
mujibu wa Mwambije mwenyewe, tukio hilo la aibu lilijiri kwenye gesti
moja iliyopo eneo la Makao Mapya jijini hapa ambayo jina linahifadhiwa
kwa sasa huku mfumaniaji huyo na timu yake wakishughulika na
mfanyabiashara huyo waliyedai ni mgoni wao.
Madai
hayo yanasema kuwa, mfanyabiashara huyo alishushiwa kipigo cha haja
baada ya kukutwa ndani ya gesti hiyo, tena akiwa mtupu na mke wa rafiki
yake huyo anayefanya kazi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ‘NSSF’ jijini hapa.
Akizungumzia tukio hilo huku akiwa na uso wenye maumivu ya hisia, Mwambije alisema kuwa, Hashimu alikuwa rafiki yake mkubwa (urafiki umekufa) ambapo wakati yeye anafunga ndoa na Felista, alishiriki kumsaidia katika shughuli za hapa na pale.
Akishushiwa kichapo.
Mwanaume
huyo aliendelea kudai kuwa, baada ya ndoa, maisha na mkewe yaliendelea
lakini hivi karibu, alishangaa kupata habari kutoka kwa watu aliokataa
kuwataja majina kwamba, rafiki yake huyo anatoka na shemeji yake.
“Nilishangaa
sana, lakini pia nilishtuka. Kwani Hashim ni rafiki yangu kipenzi.
Taarifa nilizozipata ni kwamba, amekuwa akimtongoza mke wangu tangu
mwaka jana (2014) kwa kumtumia meseji (SMS) za mapenzi.”
Mwambije
alisema baada ya kusikia taarifa hizo, alimbana mkewe, akakiri.
Akajiongeza adhabu gani ampe rafiki yake huyo, akaona hakuna nyingine
zaidi ya kumwandalia fumanizi la kukata na shoka kwa kuandaa mtego
kupitia jamaa zake na kulishirikisha jeshi la polisi.
Kwa
kauli ya Mwambije, ina maanisha kwamba kulikuwa na ushirikiano mkubwa
kati yake na mkewe, Felista ili kufanikisha fumanizi hilo.
Mwambije
alisema siku ya tukio, Mei, 10, mwaka huu, majira ya saa 7 mchana yeye
na ‘skwadi’ yake walivamia kwenye gesti hiyo na kuwanasa wawili hao
wakiwa watupu huku Felista akifanikiwa kuchoropoka na kutokomea
kusikojulikana.
Akisimulia
mazingira ya tukio la unasaji, mwanaume huyo alisema, awali rafiki yake
huyo aliwasiliana na mke wake majira ya mchana na kukubaliana kukutana
eneo hilo na kwamba baada ya kufika na kuingia chumbani mkewe, alimkuta
jamaa akimsubiri kwa shangwe kama siyo nderemo.
Mwambije
alisema mkewe baada ya kufika ndani ya chumba cha gesti, aliagiza
chipsi kuku kwanza na kuomba akaoge kabla ya kuingia kwenye sita kwa
sita akiwa ndani ya kanga moja tu ili kuvuta muda wa mumewe kufika!!
Muda
mchache wakiwa watupu, mume na timu yake, sanjari na polisi walivamia
chumba hicho na kumtoa nje mtuhumiwa huyo na kuanza kumwangushia kipigo
cha hasira za; ‘kwa nini unaniibia mke wangu?’ Licha ya urefu na uimara
wa mwili, mtuhumiwa huyo hakuonekana kufanya makeke zaidi ya kuelemewa.
Hata
hivyo, wakati wa kipigo hicho, polisi walifanya kazi ya ziada kuzuia
hasa baada ya kumsikia, mwana timu mmoja akisema maneno ya kuashiria
kutaka kumfanyia kitu mbaya mtuhumiwa huyo.
Akizungumza
na na gazeti la Amani kwa njia ya simu kuhusiana na tukio hilo,
Felista alikiri kukutwa chumba cha gesti na rafiki huyo wa mumewe na
kusema kuwa, alilazimika kumweleza mumewe kuhusu jamaa huyo kutokana na
usumbufu aliokuwa akiupata kutoka kwa rafiki yake.
...Akiingizwa kwenye gari la polisi.
Alisema: “Huyo
bwana amekuwa akinitongoza kwa muda mrefu sana. Tena amekuwa akiniambia
niombe talaka yeye atanioa kwa vile mume wangu hana pesa za kunitunza.
“Jumamosi
alinipigia simu, nikamwambia mumewe wangu, nikatoka kwetu Ilboru kwa
kupanda usafiri wa Toyo na kumfuata mahali aliponielekeza. Nilimkuta
ameshavua nguo na kubaki na shuka la gesti, ndipo mume wangu na wenzake
walipovamia,” alisema mwanamke huyo.
Hata
hivyo, katika Kituo Kikuu cha Polisi, mtuhumiwa huyo aliachiwa kwa
dhamana huku akipangiwa tarehe ya kurudi tena kituoni hapo.
Chanzo: Gazeti la Amani/Gpl
Chanzo: Gazeti la Amani/Gpl
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269