Makundi
hasimu ya wanajeshi yanakabiliana katikati ya mji mkuu wa Burundi-
Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais
Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
Redio na runinga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.
Kwa
mujibu wa taarifa ya habari ya DW mchana huu, rais
Nkurunzinza ametoa tamko fupi kupitia ukurasa wa twitter wa
rais akiwataka wananchi wa Burundi kuwa watulivu.
Taarifa ya DW pia imearifu kuwa Mkuu wa majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo ametangaza kuwa jaribio hilo limefeli.
Hata hivyo,Mkuu
wa zamani wa idara ya upelelezi ya Burundi Meja Jenerali Godefroid
Niyombare ambaye ndiye aliyeongoza mapinduzi hayo amesema kuwa
hizo ni propaganda tu za baadhi ya wanajeshi watiifu kwa rais
Nkurunzinza.
Niyombare
amesema kuwa kama ni kweli mapinduzi yamefeli, basi rais
Nkurunzinza arudi nchini leo,asiporudi leo basi hakuna haja ya
kubishana juu ya uwepo wa mapinduzi hayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269