Baadhi ya Wachezaji wa Taifa Stars baada ya kuwasili Afrika kusini
TIMU ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili leo mchana majira ya saa 6
kamili katika jiji la Rustenburg na kufikia katika hoteli ya Hunters
Rest – Protea iliyoypo pembeni kidogo ya jiji.
Taifa
Stars ambayo iliondoka jana joni jijini Dar es salaam jijini Dar es
salaam na kufika OR Tambo saa 5 usiku, ilipata mapokezi mazuri kutoka
kwa waandaji wa michuano ya COSAFA pamoja na watanzania wanaoishi jijini
humo, ililala katika hoteli ya Southern Sun.
Safari ya
kutoka Johannesburg kuelekea Rustenburg ilichukua takribani masaa
mawili na msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF Ephaphra Swai.
Baadhi ya Watanzania waishio Afrika kusini walijitokeza uwanja wa Ndege kuipokea Taifa Stars
Wachezaji
waliopo na timu Rutsenburg ni Deogratius Munish, Mwadini Ali, Shomari
Kapombe, Erasto Nyoni, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Salim Mbonde, Aggrey
Moriss, Joram Mgeveke, Said Juma, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdi
Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibhrami Ajib, Juma Luizio, John Bocco, Mrisho
Ngasa na Saimon Msuva.
Kikosi
cha Taifa Stars kinatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa
Rustenburg Impala Bowling Club majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za
Afrika Kusini sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.
Watanzania walijitokeza kuipokea Taifa Stars
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269