Bi Moza akiwa akimshindikiza mtoto wake Moh'd Saidi, Nchini India kwa matibabu Bi
Moza Moh'd Khamis anapenda tena kutoa shukurani za dhati kwa wale wote
waliochangia kwa hali na mali kwa mtoto wake Moh'd Said Moh'd, kwenda
kufanyiwa matibabu ya upandikizaji wa figo, nchini India.
Mapema
asubuhi ya jana Bi Moza aliongea na blog ya swahilivilla ili kutoa
taarifa kwa kukamilika safari yake ya kwenda nchini India pamoja na
kutaka tumuombe Dua za kumtakia kila la kheri katika safari hiyo.
Moh'd
Said Moh'd ameondoka jana Jumanne Juni 9, katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea Nchini India
kwaajili ya matibabu yake.
Napenda
kuchukua fursa hii kwa niaba ya Tanzania Bloggers Network (DMV) na
waTanzania wote waishio Nchini Marekani, kumtakia kila la kheri Ndugu
yetu Moh'd Said Moh'd katika matibabu yake huko Nchini India M/Mungu amjaalie wepesi katika safari yake na ampe afuweni na mafanikio katika mipangilio yote matibabu yake. Ameen.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269