Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) wakiwasili kwenye
ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kabla ya ziara ya kuelekea
katika kijiji cha Chasimba kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF
katika wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Bagamoyo
SERIKALI
ya Hispania imetoa shilingi bilioni 3.1 kusaidia miradi ya maendeleo ya
jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii, TASAF.
Fedha
hizo zimetolewa kupitia mfuko wa maendeleo endelevu (SDGF) zilizotolewa
kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake hapa
nchini.
Mashirika
hayo ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ,Shirika la
Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) , Shirika la Umoja wa Mataifa la
Idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la Kazi Duniani( ILO).
Hayo
yamesemwa katika ziara ya Balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis
na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez
katika kijiji cha Chasimba kilichopo wilayani Bagamoyo, Pwani jana.
Ziara
yao ilikuwa ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya
Bagamoyo. Bagamoyo ni miongoni mwa wilaya nane zilianza kupokea fedha za
TASAF na kuonekana kuleta mabadiliko makubwa katika jamii.
Hata hivyo moja ya shughuli wanazofanya wakazi wa Chasimba ni kilimo wakiwa na pato la sh 350,000 kwa mwaka.
Huduma za jamii zinazopatikana katika vijiji hivyo ni pamoja na shule ya msingi, barabara inayopita kijiji ni hapo na zahanati.
Wakati
wa utekelezaji wa awamu ya pili ya TASAF jamii ya Chasimba ilijenga
madarasa matatu na ofisi ya walimu. Miradi hiyo ilizinduliwa mwaka 2007
na kukamilika mwaka 2008. Katika miradi hiyo TASAF ilichangia
30,415,471.
Aidha
kijiji cha Chasimba ni miongoni mwa vijiji 17 ambavyo vinatekeleza
mradi wa CB-CCT toka mwaka 2008/2009. Katika kipindi hicho wamepata
ruzuku ya jumla ya sh 28,325,400.
Pia
kijiji hicho kina kaya 197 zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya
maskini TASAF III (PSSN) ambapo tayari wamepewa ruzuku ya shilingi
43,227,190 katika mikupuo 9.
Akizungumza
kijijini hapo Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliishukuru
serikali ya Tanzania na Hispania kwa kufanikisha shughuli hiyo nzito ya
kusaidia jamii kukabiliana na umaskini.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya
Bagamoyo.
“
Tunashukuru serikali ya Tanzania na Hispania kwa kushirikiana kusaidia
wananchi wa Tanzania kukabiliana na umaskini. Kwa kufanyakazi na watu wa
hali ya chini kabisa miradi hii imewezesha familia kupeleka shule
watoto wao, kushiriki katika mipango ya uwekaji wa akiba na kuongeza
kipato. Jukumu letu la pamoja ni kuondoa umaskini Tanzania” alisema
Alvaro.
Naye
Balozi wa Hispania Luis amesema kwamba serikali ya Hispania inaamini
katika kusaidia kupambana na umaskini kwa kusaidia jamii kukabiliana na
changamoto zinazowakabili.
Alisema
wataendelea kufanya hivyo kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo
yanafanyakazi kwa kushirikiana na serikali za mikoa na mitaa ambazo
ndizo ziliopo karibu na wananchi husika.
Alisema kwamba wanaamini mradi wa kunusuru kaya maskini unafanya wajibu wake kwa kuwafikia wananchi maskini sana.
Alisema
mradi huo ni moja ya miradi inayoonesha umuhimu wa kufanyakazi pamoja
kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na nchi wahisani.
Kijiji
cha Chasimba pia kinafanya kazi za ujenzi mbalimbali kuanzia Machi 23,
mwaka jana. Kazi hizo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kilomita 1.1 ya
Chasimba-Kiegea.
Aidha kumekuwepo na mafanikio makubwa tangu kuanza kwa mradi wa PSSN kijijini hapo.
Alisema
kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa na kuhudhuria
shule, aidha madarasa matatu yamejengwa na ofisi ya mwalimu.
Akizungumzia
mafanikio Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga alisema kuna
mabadiliko makubwa katika maisha ya watu kutokana na utekelezaji wa
miradi hiyo katika kijiji.
Aidha
wananchi wa Chasimba wamepata ushawishi mkubwa wa kushiriki katika
miradi ya maendeleo ndio sababu ya mafanikio yanayoonekana.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopo mradi wa kunusuru kaya maskini umesaidia
watoto kwenda shuleni wakiwa wametimiziwa mahitaji yao yote.
Aidha mradi huo umeweza kufanikiwa kufanya watu wapendekwenda kiliniki na kuangalia afya za mama na watoto.
Aidha familia zilizopewa fedha sasa wamebadilisha namna ya mfumo wa kupata lishe na kuwa na uhakika na lishe.
Aidha
ujira kutokana na kazi unaotarajiwa kutolewa ni jumla ya dola za
Marekani 15,991 wakati gharama za vifaa na ufundi ni dola za Marekani
5,328.
Jumla
ya kaya 197 zitashiriki katika miradi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi
minne na utaendelea kwa miaka miwili katika kipindi hicho hicho.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia), Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) pamoja na Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (katikati) wakielekea kwenye
ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kupokea taarifa ya mradi wa TASAF katika
wilaya ya Bagamoyo.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (wa pili kushoto) akifafanua
jambo kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi ya TASAF
katika wilaya ya Bagamoyo kwa wadau wa maendeleo waliotembelea wilaya
hiyo kukagua miradi inayofadhiliwa na Tasaf. Kulia ni Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez sambamba na Balozi wa Spain
nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kulia) na kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa wilaya ya Bagamoyo, Hilda Gadi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga
akizungumza kwenye mkutano mfupi wa kupokea taarifa ya miradi
inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo. Wa pili kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi, Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (katikati), Balozi wa Spain
nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi akitoa
taarifa ya maendeleo ya mradi wa TASAF wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini katika wilaya ya Bagamoyo mbele ya wadau wa maendeleo.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis akizungumzia ufadhili wa
serikali yake kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini ambayo
mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza
katika mkutano huo ambapo aliishukuru serikali ya Tanzania na
Hispania kwa kufanikisha shughuli ya kusaidia jamii kukabiliana na
umaskini ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Malengo ya Millenia (MDG's).
Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa TASAF wakishiriki kwenye mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (katikati) akijadiliana jambo na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia)
pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (kushoto).
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) akiteta jambo na Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi. Kushoto
ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269