Ofisa
Uhusiano wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafarri
Malema (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo
(hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli
zinazofanywa na Rita na umuhimu wa cheti cha kuzaliwa. Kulia ni Ofisa
Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi.
Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi akizungumza katika mkutano na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo.
Wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo wakiwasikiliza maofisa wa Rita walipokuwa wakizungumza nao.
Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa kwani vina umuhimu katika maisha ya kila siku ndani na nje ya nchi.
Mwito
huo umetolewa na Ofisa Uhusiano wa Wakala wa Usajili Ufilisi na
Udhamini (RITA), Jafarri Malema wakati akizungumza na wafanyakazi wa
gazeti la Jambo Leo Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli
zinazofanywa na Rita na umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa.
"Cheti za kuzaliwa ni msingi wa mafanikio ya kila mmoja wetu na ni muhimu kuwa nacho" alisema Malema.
Alisema
Rita imekuwa ikifanya shughuli za usajili wa vizazi,vyeti vya kuzaliwa,
kuandika wosia, kusajili ndoa na talaka na udhamini kama mali za umma
na ile isiyokuwa na mwenyewe.
Alisema
faida ya kuandika wosia unasaidia kuepusha watoto, mke au mume
kunyang'anywa mali pale kinapotokea kifo na inawezesha kumchagua
msimamizi wa mirathi.
Alitaja
faida nyingine ya kuandika wosia kuwa ni kuepusha migongano katika
familia, ndugu au jamaa na kuwa unampa uhakika wa maisha bora ya baadae
warithi wa mali waliziachiwa.
Alisema
jambo linalofanyika baada ya kufariki kwa mtu aliyeandika wosia mmoja
wa mashahidi anatakiwa kwenda kutoa taarifa Rita ambapo taratibu za
wosia kuwasilishwa mahali husika hufanyika.
Naye
Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi alisema umuhimu wa kuwa na cheti
cha kuzaliwa ni mkubwa kwani ni nyaraka pekee yenye mamlaka kisheria
kuthibitisha tarehe na mahali mtu alipozaliwa na ni nyaraka muhimu kwa
kila mwananchi kwani hutumika kupata huduma nyingine za msingi kama
elimu, afya na makazi.
Alisema
cheti cha kuzaliwa kinawawezesha watoto kujiunga na elimu ya msingi na
sekondari na kuwawezesha kupata nafasi ya masomo ya elimu ya juu pamoja
na mikopo ya masomo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269