Breaking News

Your Ad Spot

Mar 1, 2016

KERRY : US, RUSSIA ZINALENGA DAESH NA AL-NUSRA SYRIA

Kerry: US, Russia zinalenga Daesh na al-Nusra Syria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amesema kuwa Washington na Moscow zimekubaliana kutojadili madai ya kukiuka makubaliano ya usitishaji vita nchini Syria ambayo yalianza kutekelezwa hivi karibuni na kuongeza kuwa vikosi vya nchi mbili hizo vitalenga tu kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh na al-Nusra katika mashambulizi yao.
Katika kikao na waandishi wa habari jana Jumatatu nchini Marekani, John Kerry ambaye wakati wa hotuba hiyo alikuwa pamoja na mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amesema amekubaliana na mwenzake wa Russia, Sergei Lavrov juu ya kuunda ramani ya njia itakayohakikisha kuwa mashambulizi ya vikosi vyao yanalenga tu matakfiri wa Daesh na al-Nusra. Kerry amesema timu za mazungumzo za Geneva huko Uswisi ndizo zitakazojadili kadhia hiyo ya kukiukwa makubaliano ya usitishaji vita. Umoja wa Mataifa umesema makubaliano ya usitishaji vita yanatekelezwa katika maeneo mengi ya Syria. Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema kuwa Saudi Arabia inapanga njama ya kuvuruga makubaliano hayo. Aidha Russia imeituhumu Uturuki kuwa imekiuka makubaliano hayo, baada ya duru za habari kuripoti kuwa nchi hiyo ndiyo iliyohusika katika hujuma ya hivi karibuni katika mkoa wa Latakia, kaskazini mwa Syria.
Wakati huo huo, serikali ya Moscow imesema kuwa, kufuatia mashauriano na mazungumzo ya kina, huenda chaguo la kuanzisha serikali ya kifederali nchini Syria likawa dawa mjarabu ya mgogoro wa Syria.
Katika kipindi cha karibu miaka mitano ya hujuma za magaidi Syria, takribani watu 470,000 wamepoteza maisha na mamilioni ya wengine kuachwa bila makazi.
K

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages