Rais wa Gabon Ali Bongo amesema atawania kuhifadhi kiti chake kwa
muhula wa pili katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika baadaye mwaka
huu.
Rais Bongo alitoa tangazo hilo jana Jumatatu alipolitembelea eneo
lenye utajiri wa mafuta la Port Gentil, ambalo limekuwa likionekana kama
ngome ya upinzani nchini humo. Katika hotuba yake hiyo, Rais wa Gabon
alisema kuna haja ya kukabiliana na kile alichokitaja kuwa mfumo wa
unyonyaji, ambapo watu wachache pekee ndio wenye kustafidi na utajiri wa
mafuta wa nchi hiyo ya Afrika. Ali Bongo ambaye aliingia madarakani
mwaka 2009 baada ya kifo cha baba yake, Omar Bongo ambaye aliitawala
nchi hiyo tokea mwaka 1967; anatazmiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa
kiongozi wa upinzani Jean Ping, mwanadiplomasia maarufu wa Gabon ambaye
alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kutoka mwaka 2008 hadi
2012. Wananchi wa Gabon wamekuwa wakifaya maandamano mara kwa mara,
kulalamikia ugumu wa maisha na tuhuma za kukandamizwa viongozi wa
upinzani na wakosoaji wa serikali.
Uchaguzi mkuu nchini Gabon unatazamiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka
huu, ingawa tarehe ya uchaguzi huo bado haijaainishwa na vyombo husika
hadi sasa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269