Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kujitokeza kwa
wingi wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu katika uchaguzi wa Ijumaa
iliyopita ni ithibati tosha kuwa taifa la Iran linatii miito ya Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kutuma ujumbe wa kufeli
njama za mabeberu dhidi ya taifa hili.
Ayatullah Sadeq Amoli Larijani amewapongeza wananchi wa Iran kwa
kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Bunge la 10 la Jamhuri ya
Kiislamu na wa 5 wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Ayatullah Larijani amesema uchaguzi
wa Februari 26 umetuma ujumbe kwa dunia kwamba taifa la Iran lingali
linafungamana na mfumo wa Mapinduzi ya Kiislamu na miongozo ya Kiongozi
Muadhamu, Ayatullah Ali Khamenei. Akiashiria propaganda zilizoenezwa
kabla ya uchaguzi na vyombo vya habari vya Marekani na Uingereza, Mkuu
wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, taifa hili limeonyesha
kuwa haliwezi kuhadaiwa na maadui wake ili kubadili misimamo yake.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran, asilimia 62 ya
wananchi milioni 55 waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki
katika uchaguzi huo wa Ijumaa iliyopita.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269