Saudi Arabia inashirikiana kikamilifu na utawala haramu wa Israel
katika njama ya kuomuondoa marakani Rais Bashar al-Asad wa Syria pamoja
na kuwepo mapatano ya usitishwaji vita nchini humo.
Imedokezwa kuwa viongozi wa ngazi za juu wa Saudi Arabia wametembelea Israel kwa siri katika kipindi cha siku chache zilizopita.
Shirika la Habari la Sputnik News la Russia liliandika Jumapili ya
jana kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Adel Al Jubeir na
Khalid Al Hamidan Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Saudia wametembelea
Israel kwa siri.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wawili hao walikuwa na ujumbe maalumu wa
kiusalama ambao ulihusu oparesheni za kijeshi dhidi ya Syria na Lebanon.
Uamuzi huo ulichukuliwa katika mkutano wa maafisa wa ngazi za juu wa
Saudia na wakuu wa utawala haramu wa Israeli akiwemo mkuu wa shirika la
ujasusi la utawala huo, Mossad. Aidha imedokezwa kuwa katika safari hiyo
ya siri, Al Jubeir pia amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu
wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu.
Sputknik imefichua kuwa, lengo kuu la safari ya Adel Al Jubeir huko
Israel ni ombi la Saudia kwa Israel kuingilia moja kwa moja kijeshi
kusini mwa Syria kupitia hujuma ya nchi kavu ili kuishinikiza kijeshi
Syria.
Gazeti la Financial Times la Uingereza pia wiki iliyopita liliripoti
kuwa Saudi Arabia inataka kutekeleza hujuma ya kijeshi dhidi ya Syria
kwa ushirikiano na Uturuki.
Watawala wa Saudia wangali wanafuatilia njama ya kumuondoa madarakani
Rais Bashar al Assad wa Syria pasina kutumia njia za kisiasa na
mazungumzo ya amani. Ni kwa msingi huo ndio maana utawala wa Kizayuni wa
Israel ukaunga mkono njama hizo za Saudia kwa matumaini kuwa huo
utakuwa mwanzo wa kusambaratika mstari wa mbele wa mapambano katika eneo
la mashariki ya Kati. Tokea uanze mgogoro wa Syria, magaidi wanaopigana
dhidi ya serikali ya Damascus wamekuwa wakipata matibabu katika
hospitali za Israel zilizo katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Milima
ya Golan.
Aidha maafisa wa jeshi la Israel wamekuwa wakiwapa mafunzo ya kijeshi magaidi wa makundi ya ISIS au Daesh na Jabhatu Nusra.
Kufichuka safari ya siri ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia huko
Israel pamoja na matamshi ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani John Kerry kuwa iwapo usitishaji vita Syria utafeli basi kuna
mpango mbadala ni mambo yanayoashiria kuwepo ushirikiano wa karibu kati
ya Marekani, Israel na Saudia katika njama dhidi ya Syria. Ni wazi kuwa
pande hizo tatu zinatekeleza njama za kumuondoa madarakani Rais Assad
kwa kutumia njia zozote zinazowezekana.
Kumeibuka wasiwasi wa kutofanikiwa mapatano ya utekelezwaji mapatano
ya usitisahji vita Syria kutokana na matamshi ya John Kerry. Hujuma ya
kijeshi ni kati ya mpango mbadala wa Marekani iwapo utafeli mchakato wa
kisiasa katika kutatua mgogoro wa Syria.
Weledi wa mambo wanasema katika safari yake ya siri Israel, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Saudia alijadili na Wazayuni njia za kuwapa nguvu
magaidi Syria katika kipindi hiki cha wiki mbili za usitishwaji vita.
Miaka mitano ya mgogoro wa Syria na kusimama kidete taifa la Syria na
Rais Assad mbele ya njama za magaidi na waitifaki wao ni jambo
linaloashiria kuwa, kumuangusha Assad si chaguo rahisi kwa Saudia,
Uturuki na Israel
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269