Breaking News

Your Ad Spot

Jul 10, 2016

MADUKA YA WATU WENYE ASILI YA ASIA NCHINI KONGO DR, YAFUNGULIWA CHINI YA ULINZI WA POILSI

Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeimarisha usalama kwenye maduka ya biashara ya watu wenye asili ya Asia mjini Kinshasa, mji mkuu wa nchi hiyo kufuatia kujiri maandamano na mashambulizi ya Wakongomani dhidi ya maduka hayo.
Duru za usalama nchini humo zimearifu kwamba, serikali ya nchi hiyo imetaka kuimarishwa usalama katika maduka hayo sanjari na kuendelea kuwepo askari katika maeneo hayo ya biashara ya watu wenye asili Asia. Hii ni katika hali ambayo maduka mengi ya wafanyabiashara hao yalifungwa kwa siku mbili kufuatia vurugu za Wakongomani zilizozuka mjini Kinshasa dhidi ya wafanyabiashara ha kwa kile walichokitaja kuwa ubaguzi wa rangi unaofanyiwa wenyeji wa nchi hiyo. Habari zinaripoti kwamba, vurugu hizo ziliizuka baada ya mke wa mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya Asia kumuua mwanamke mwingine raia wa Kongo DR nchini India. Ijumaa iliyopita, afisa mmoja wa ubalozi wa India nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alikutana na familia ya mwanamke aliyeuawa na ile ya mke wa mfanyabiashara mwenye asili ya India, baada ya kiongozi mmoja wa serikali kuutaka ubalozi huo kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages