Breaking News

Your Ad Spot

Jul 10, 2016

WAMAREKANI WAENDELEA KPINGA UBAGUZI WA RANGI NA UKATILI WA POLISI

Marekani imegubikwa na wingu zito la maandamano ya wananchi wanaopinga ukatili na mauaji yanayofanywa na polisi wazungu dhidi ya raia wenye asili ya Afrika.
Ukatili huo umechochea mauaji yaliyofanyika siku chache zilizopita ya polisi watano katika mji wa Dallas, tukio ambalo linahusishwa na ghasia na mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Habari ya kupigwa risasi maafisa 11 wa polisi katika mji wa Dallas na kuua polisi wasiopungua 5 miongoni mwao imeitikisa sana Marekani na kuzusha maswali mengi katika fikra za watu dunia kuhusu ubaguzi wa rangi na ukatili na utumiaji mabavu unaotawala jamii ya Marekani. Kumekuwepo pia habari za kutatanisha kwamba waandamanaji wanaopinga ukatili wa polisi wamevamia majengo ya Congresi ya nchi hiyo na kwamba mabomu kadhaa yametegwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dallas.
Katika matamshi yake ya awali kuhusu malalamiko ya wananchi katika mji wa Dallas na yanayojiri katika eneo hilo, Rais Barack Obama anayeshiriki mkutano wa NATO huko Poland amesema kuwa, wananchi wote wa Marekani wana wasiwasi kuhusu muaji yanayofanywa na maafisa wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi.
Kanali mbalimbali za habari za Marekani zimekuwa zikitangaza na kutoa ripoti za matukio na machafuko ya miji mbalimbali ya nchi hiyo. Vilevile maafisa wa Idara ya Usafiri wa Anga ya Dallas wamepiga marufuku safari za ndege katika anga ya mji huo. Gazeti la Washington Post pia limetahadharisha kuhusu ongezeko la mauaji yanayofanywa na polisi ya Marekani dhidi ya raia.
Wimbi la sasa la maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani lilianza baada ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuonesha picha na video za ukatili wa polisi na mauaji ya Wamarekani wawili weusi. Maelfu ya Wamarekani walianza kufanya maandamano Alkhamisi iliyopita katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kupinga ubaguzi dhidi ya raia wenye asili ya Afika. Picha za mauaji ya kikatili ya Philando Castile na Alton Sterling, zimewamimina mitaani Wamarekani katika miji kama Washington, Los Angeles, Chicago na New York asaa wakafikisha sauti na malalamiko yao kwa viongozi wa nchi hiyo wakipinga ubaguzi na ukatili wa polisi. Waandamanaji wengi walibeba mabango yenye maandishi: 'Maisha ya watu weusi yana thamani'.
Gavana wa jimbo la Minnesota, Mark Dayton amesema baada ya mauaji ya kijana wa pili mweusi katika mji huo kwamba: Hakika haya ni maafa ya kutisha kwa watu wa Minnesota hususan familia na marafiki wa Philando Castile. Mmarekani huyu mweusi alipigwa risasi na kuuliwa na polisi alipokua akitaka kuonesha leseni yake baada ya kusimamishwa barabarani akiwa pamoja na mchumba na mtoto wake.
Polisi wazungu wa Marekani daima wamekuwa wakitumia visingizio mbalimbali kuhalalisha mauaji ya raia hususan wenye asili ya Afrika. Mwaka jana pekee zaidi ya raia elfu moja waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi ya Marekani wengi wao wakiwa Wamarekani weusi.
Hivi karibuni Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch alikiri kwamba, ukatili wa polisi ni tatizo kubwa nchini humo. Lynch alisisitiza kuwa mwenendo wa polisi na raia si mzuri na wakati mwingine huwa ni wa kinyama.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages