Ujumbe huo uliwasilishwa jana jijini Dar es Salaam na Mjumbe Maalum wa Rais Nyusi Meja Jenerali Mstaafu Mariano de Araujo Matsinhe ambaye aliongozana na Mshauri wa Diplomasia wa Rais Nyusi, Kanali Manuel Mazuze, Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Monica Patricip Clemente Mussa na Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini Rachide Usualle.
Katika Ujumbe huo, Rais Nyusi amemuomba Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kushiriki mazungumzo ya amani nchini Msumbiji, ambapo Dk. Kikwete amekubali.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na ujumbe wa Rais Filpe Nyusi uliofika kuwaslisha ujumbe maalum jijini Dar es Salaam jana
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269