Raia
wa Afrika Kusini waliopanda Mlima hivi karibuni kwa lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua taulo za kusaidia watoto wa
kike.aliyechuchumaa mbele (mwenye kofia) Gugu Zulu ndiye anatajwa
kufariki Dunia wakati akielekea Kileleni.
Gugu Zule (Kulia) akiwa na Richard Mabaso muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Gugu
Zulu akiwa katika lango la Marangu akipata picha na mmoja wa washiriki
wa safari hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.
Gugu
Zulu (kushoto) akiwa na rafiki yake muda mfupi kabla ya kuanza safari
ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika kampeni ijulikanayo kama
Trek4Mandela ikiwa na lengo la kchangisha fedha kwa ajili ya kunua taulo
za watoto wa kike pamoja na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa
baba wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
Ra
ia wa Afrika ya Kusini Guguleth Mathebula Zulu
(38) aliyefika nchini kwa ajili utalii wa
kupanda Mlima Kilimanjaro amefariki leo tarehe
18.7.2016 baada ya kupatwa na tatizo la
kushindwa kupumua kwenye mwinuko wa juu mlimani.
Shirika
la Hifadhi za Taifa nchini kwa kushirikiana na
mamlaka mbalimbali za serikali zinaendelea na
uratibu wa kurejesha mwili wa marehemu nchini
Afrika ya Kusini kwa ajili ya taratibu za
maziko.
Zulu
alifika nchini na kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro
tarehe 14.7.2016 kwa ajili ya kuenzi jitihada
za Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini
Nelson Mandela za kusaidia familia maskini nchini
Afrika ya Kusini, hususani kuwapatia mahitaji
muhimu watoto wa kike ambao hawana uwezo wa
kupata mahitaji muhimu.
Hii
ni mara ya pili kwa watalii kutoka Afrika ya
Kusini kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya
kuenzi juhudi za Mandela katika kusaidia jamii
ya watoto wa kike kupitia kampeni maalum ya
kupanda Mlima Kilimanjaro.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano Hifadhi za Taifa Tanzania
S.L.P 3134
Baruapepe: dg@tanzaniaparks.go.tz
Wavuti: www.tanzaniaparks.go.tz
18.07.201
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269