Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema
kuwaangamiza magaidi katika mji wa Aleppo, kaskazini magharibi mwa nchi
ndio chagua la pekee na la kisheria la kuwadhaminia usalama raia.
Assad ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni
ya SRF 1 ya Uswisi na kuongeza kama tunavyomnukuu: "Lengo letu ni
kuwafurusha na kuwaangamiza magaidi wanaohatarisha usalama wa raia
katika mji wa Aleppo na jukumu hilo tumepewa na wananchi kupitia sheria
na katiba."
Kiongozi wa taifa la Syria ameongeza kuwa, njia pekee ya
kuwahakikishia wananchi usalama katika mji wa Aleppo ni kuwaangamiza
magaidi wa Daesh ambao walikuwa wameugeuza mji huo kuwa ngome yao.
Jeshi la Syria likisaidiwa na jeshi la anga la Russia hivi karibuni
lilianzisha oparesheni kubwa ya kijeshi kwa minajili ya
kuwatimua magaidi katika mji wa Aleppo na hadi sasa magaidi wa Daesh na
wa makundi mengine ya kigaidi zaidi ya 1000 wameuliwa na wengine karibu
2500 kujeruhiwa.
Wiki iliyopita, Rais Bashar al-Assad wa Syria alisema kuwa:
"Tunaamini Aleppo ni pacha wa Damascus kwa sababu kadhaa, kwanza ni mji
wa pili kwa ukubwa nchini Syria. Damascus ni mji mkuu wa kisiasa, katika
hali ambayo Aleppo ni mji mkuu kiuchumi. Kwa ajili hiyo kuukomboa mji
huo kuna maana ya kujiimarisha zaidi kiuchumi na kisiasa."
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269