Habari picha na Woinde Shizza, Arusha
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amezusha vurugu kwa kutaka kupigana na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa sababu ya kutaka apewe 'ujiko' katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya Buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.
Lema, alizusha vurugu hizo, mara Mkuu wa mkoa, alipokaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Alexanda Mnyeti, kutoa hotuba, lakini baada ya kuanza kuhutubia akielezea historia ya mradi huo ikiwemo upatikanaji wa eneo la ujenzi, ghafa Lema alisimama na kupaza sauti hovyo kupinga akidai maelezo ya mkuu huyo wa mkoa hayakuwa sahihi.
Badala ya Lema, kusubiri Mkuu huyo wa mkoa amalize hotuba, yake, naye alizidi kupaza sauti akidai kwamba yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi katoka kampuni ya Mawala Advocate na kudai kuwa si kweli kwamba kupatikana kwa eneo hilo kumetokana na maono aliyokuwa nayo marehemu Advocate Nyaga Mawala kwa mda mrefu kama alivyoeleza mkuu wa mkoa wakati akihutubia.
Lema alianza kuonekana kuingiwa kinyongo, baada mkuu wa mkoa Mrisho Gambo kupewa nafsi ya kutangulia kuongea kabla yake na wafadhili, kama ambavyo ratiba ya awali ilivyokuwa imepangwa katika uzinduzi wa mradi huo uliofadhiliwa na shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto linalofahamika kwa jina la Maternity Afrika.
“Mkuu wa mkoa acha kupotosha uma , mchungaji simamisha hutuba ya mkuu wa mkoa anavoongea siyo kwa kweli, sitakubali huu uongo uendelee, akitaka atumie nguvu ya polisi siogopi kufa....", alisikika Lema akisema kwa sauti kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa.
Taharuki hiyo liliwalazimu baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo kinamama kumsihi mbunge huyo kupunguza jazba kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa hali ambayo ingeweza kusabisha uvunjifu wa amani.
Licha ya vurugu hizo Mkuu wa mkoa wa Arusha aliendelea kuhutubia akiwa anaeleza kuwa eneo hilo lilitolewa na marehemu Nyaga Mawala kwa serekali ili liendelezwe kwa kujengwa hospitali ya huduma ya mama na mtoto.
“hili jambo sio la siasa tusiingize siasa, na kama kunamtu anampango wa kufanya siasa hapa anapoteza muda wake mimi ni mkuu wa mkoa na ninafahamu historia ya eneo hili”alisema Gambo
Kwa upande wake mfadhili wa maradi huo ambaye ni Daktari Bigwa wa magonjwa ya Festula Duniani Dk.Edru Broun alieza kusikitishwa na tukio lilijitokeza na kuwataka viongozi waweke pembeni siasa zao na tofauti zao na wamtangulize mungu ili kutimiza shabaha ya ujenzi wa kituo hicho cha hospitali kitakachoweza kumsaidi mama na mtoto.
Alisema kuwa ujenzi wa hopitali hiyo utagharimu jumla ya sh. bilioni 6 na kwamba katika awamu ya kwanza kiasi cha sh. bilioni tatu kitatumika..
Your Ad Spot
Oct 18, 2016
Home
Unlabelled
GODLBESS LEMA AZUSHA VURUGU HAFLA YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI WA HOSPITALI YA MAMANA MTOTO
GODLBESS LEMA AZUSHA VURUGU HAFLA YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI WA HOSPITALI YA MAMANA MTOTO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269