Mhandisi
wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mkoa John Kalupale (kwanza kulia)
akiwatambulisha wawakilishi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture
Ltd walipokuja kukabidhi msaada wa mabati na Cement kwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha.
Maneja
Mradi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, Bw.Xie (kulia
mbele) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mbele kushoto)
mfuko wa saruji na bati kama sehemu ya msaada wa bati 500 na mifuko ya
saruji 500 waliyoitoa kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za
Maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo (mbele) akishukuru Kampuni ya
Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd kwa kutoa msaada kwa wananchi wa Arusha.
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(mbele kushoto) akikabidhi Mkuu wa
Wilaya ya Arusha mifuko ya saruji 100 na bati 100 kwa ajili ya Ujenzi wa
Kituo cha Afya Muriet.
Mbunge wa
Viti Maalum Mkoa wa Arusha kupitia Tiket ya Ccm Catherine Magige(kwanza
kushoto) akitoa shukrani kwa kampuni ya Ujenzi iliyotoa msaada kwa
ajili ya kuwezesha huduma za kijamii Mkoani Arusha.
Mbunge wa
Viti Maalum anayewakilisha Kundi la Walemavu kupitia Tiket ya Ccm Amina
Mollel(kwanza kushoto) pia alitoa shukrani zake kwa kwa Kampuni
iliyotoa msaada.
Mkurugenzi
wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia (pili kulia) akishkuru kwa msaada wa
Mabati 100 na Mifuko ya saruji 100 aliyopewa kwa ajili ya ujenzi wa
Kituo cha Afya Terrat.
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kushoto) akimshkuru Meneja wa Kampuni
ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati
500 na mifuko ya saruji 500.
Kutoka
kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel, Mkuu wa Wilaya ya Arusha
Mhe. Gabriel Daqarro pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Mhe. Catherine
Magige baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati 500 na mifuko ya
saruji 500 toka kampuni ya ujenzi wa barabara ya Sakina Tengeru na
barabara ya Mchepuko.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
MKUU wa
Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na
mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za
maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na
sekondari za Mkoa wa Arusha.
Mara
baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo,
Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko
100 ya saruji na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya
kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.
Alisema
msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za
mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na
mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.
Alimshukuru
Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil – Jiangsu Joint Venture Ltd,
inayojenga barabara ya Sakina – Tengeru Km 14.1 na barabara ya
Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada huo kama sehemu ya
kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza mahusiano na kujali jamii
na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa barabar hiyo
itakayogharimu takribani Bil. 139.
“Naishukuru
kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo na
naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya
nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto
mbalimbali kwa jamii “.
Naye
Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Bw. Xie alisema kampuni yao imeona umuhimu
wa kuchangia jamii kwani wao ni wajenzi wa barabara na wanastahili
kurejesha faida kwa jamii inayowazunguka.
Naye Mkuu
wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro alimshukuru Gambo kwa msaada
huo na kusisitiza kuwa mifuko hiyo 100 ya saruji pamoja na bati
100 zitasaidia ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa Kata ya Muriet
Jijini Arusha.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru kwa msaada huo utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na kukamilika ndani ya miezi miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha Kituo kinajengwa katia ubora unaostahili.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru kwa msaada huo utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na kukamilika ndani ya miezi miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha Kituo kinajengwa katia ubora unaostahili.
Katika
makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na wabunge wa Viti maalum wanawake
Mkoa wa Arusha, Catherine Magige na Aminah Mollel walitoa rai kwa
nyakati tofauti kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumuunga mkono Mhe. Gambo
pamoja na Serikali ili kuwezesha maendeleo kusonga mbele.(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269