Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angellah Kairuki, akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix
Lyaniva, alipowasili Ofisi za mkuu huyo kwa ajili ya kuhitimisha ziara
yake ya siku mbili kuwatembelea, kuwasikiliza na kuzungumza na wanufaika
hao wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf ) wa Manispaa za Kinondoni na Temeke jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf ) na wakazi wa maeneo ya Sandali, wakiwa katika mkutano na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, kwenye Mtaa wa Mamboleo, Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam jana.
Diwani
wa Kata ya Sandali, Temeke jijini, Abel Tarimo, akitoa maelezo kuhusu
masuala mbalimbali kwenye mtaa wake huo, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki,
alipokuwa na mkutano na wanufaika wa Tasaf pamoja na wakazi wa maeneo
hayo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angellah Kairuki (kulia), kuzungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja
na wananchi ambao kaya zao hazijaingizwa katika mpango huo. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Nasib Mbaga.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angellah Kairuki, akizungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na
wananchi wa Kata ya Sandali, ambao kaya zao bado hazijaingizwa katika
mpango huo.
Baadhi
ya watendaji wa Mkoa na waratibu wa Tasaf wa Manispaa ya Temeke wakiwa
katika mkutano huo, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki,
wakati alipokuwa akizungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi
ambao kaya zao bado hazijaingizwa katika mpango huo.
Baadhi ya waratibu wa Tasaf wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika mkutano huo.
Mmoja wa wanufaika wa Tasaf, akimpatia zawadi ya kitenge Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angellah Kairuki (kulia), baada ya kuzitumia fedha za ruzuku
anazopewa na Tasaf katika mradi wa kutengeneza bidhaa hizo.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Temeke, Feysal Salum, akizungumza na wanufaika
pamoja na wananchi ambao hawajanufaika na Tasaf, wakati wa mkutano huo,
Mtaa wa Mamboleo, Kata ya Sandali jijini Dar es Saaam.
Diwani
wa Kata ya Mtoni, Benard Mwakyembe, akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah
Kairuki, alipofika na kufanya mkutano na wanufaika wa Tasaf pamoja na
wananchi ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo, maeneo ya Shule ya
Msingi Mtoni, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi
ya wanufaika wa Tasaf katika mpango wa Serikali wa kuzinusuru kaya
masikini pamoja na wananchi ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo
wa maeneo ya Kata ya Mtoni, Temeke jijini Dar es Salaam jana,
wakisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa katika mkutano
huo.
Mkurugenzi
wa Uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Alphonce Kyariga,
akitoa ufafanuzi katika kuwapa ufahamu wanufaika wa Tasaf pamoja na
wananchi wa maeneo hayo ya Kata ya Mtoni, ambao bado hawajaingizwa
katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini. Kushoto ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah
Kairuki.
Mmoja
wa wananchi wa Kata ya Mtoni, ambaye bado kaya yake haijaingizwa katika
mpango huo, Rajab Bakari, akitoa malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah
Kairuki kuhusu kutokufikiwa na mpango huo, ilhali akiwa ni mmoja wa
watu wanaostahiki kupata ruzuku hiyo.
Mwananchi
wa Kata ya Mtoni, ambaye bado kaya yake haijaingizwa katika mpango huo,
Uwesu Thabiti, akitoa malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki
kuhusu kutokufikiwa na mpango huo, ilhali akiwa ni mmoja wa watu
wanaostahiki kupata ruzuku hiyo. (P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269