.

TANZANIA NA MAREKANI KUDHIBITI BIASHARA HARAMU YA BINADAMU

Oct 19, 2016


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Carl Fox, baada ya kumtembelea naibu katibu mkuu ofisini kwake kwa lengo la kujadili ushirikiano wa Tanzania na Marekani katika kudhibiti biashara hiyo.Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.(PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Carl Fox  akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, baada ya kumtembelea Naibu Katibu Mkuu ofisini kwake kwa lengo la kujadili ushirikiano wa Tanzania na Marekani katika kudhibiti biashara hiyo. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka wizarani , Seperatus Fella na wengine ni wajumbe walioongozana na Naibu Mkurugenzi kutoka ubalozi wa Marekani.

Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Seperatus Fella akizungumza na  Naibu Mkurugenzi kitengo cha kupambana na kuzuia usafirishaji binadamu, juu ya  hali ya biashara haramu ya usafirishaji binadamu  nchini na namna ambavyo wanashirikiana na taasisi mbalimbali  kuzuia na kutokomeza  biashara hiyo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช