Ikiwa
zimesalia siiku tano kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, utafiti
unaonyesha kuwa Hillary Clinton na Donald Trump wameendelea kukaribia.
Utafiti wa hivi karibuni unampa Donald Trump ushindi katika majimbo
kadhaa muhimu. Hali hiyo ndio imepelekea Barack Obama kuamua kufanya
kampeni kwa niaba ya Waziri wake wa zamani wa Mashauriano ya Kigeni.
Mwaka
2008, 90% ya wapiga kura weusi walimpigia kura Barack Obama. Miaka
minane baadaye, Wamarekani weusi hawajahamasishwa vya kutosha kwa
kumpigia kura Bi. Hillary Clinto ambaye anataka kumrithi rais
anayemaliza muda wake.
Kwa muda
wa siku tano zinazosalia, rais anayemaliza muda wake atakua akifanya
kampeni katika majimbo ya North Carolina, Ohio na Florida, jambo ambalo
si la kawaida katika kampeni ya urais. Na Rais Barack Obama ameweka
matumaini yake makubwa kwa Wamarekani weusi.
Jumatano,
Novemba 2, Obama alikuwa alialikwa na Tom Joyner katika kipindi cha
Morning Show kinachorushwa kwenye radio kila siku asubuhi, ambpo
walishiriki kwa kiasi kikubwa Wamarekani weusi. "Kura za Wamarekani
weusi si imara kama ambavyo inelipaswa kuwa. Najua kuwa watu wengi
katika vinyozi, katika maduka ya vipodozi au katika vitongoji wanakoishi
Wamarekani weusi wanampenda Barack. Wanampenda Michelle. Lakini unajua
nini? Kila mmoja wenu anapaswa kuelewa kwamba kila kitu ambacho tumeweza
kufanya kinategemea sasa na uwezo wangu wa kumkabidhi mwenge mtu ambaye
anafuata viwango sawa na mimi, " amesema Rais Barack Obama.
Kwa hiyo
Barack Obama hafanyi kampeni kwa niaba ya Hillary Clinton. Lakini pia
anajaribu kuokoa urithi wake wa kisiasa ambao Donald Trump amekwisha
kuahidi kuuondoa atakapopata ushindi.
■ Uchunguzi barua pepe: Obama aonyesha msimamo wake
Rais wa
Marekani Barack Obama ameonya kuwa uchunguzi wa shirika la kijasusi la
FBI kuhusu barua pepe za Hillary Clinton usiendeshwe kwa njama za
kumuangusha wala za kumkashifu.
Maneno ya
Obama yanaonekana kama ukosoaji ambao si wa moja kwa moja kwa
mkurugenzi wa shirika la upelelezi la FBI, James Comey. James Comey
alitangaza wiki iliyopita kuwa shirika hilo limeanza tena uchunguzi
baada ya kupokea barua pepe ambazo zinaweza kuwa za muhimu.
Obama amemwaambia waandishi wa Marekani kwamba anaimani kamili juu ya mgombea urais wa Democratic.RFI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269